MSANII NANDI KUNOGESHA MISS TANZANIA KANDA YA KASKAZINI KESHO ARUSHA - JAMII BLOG

Jamii Yetu , Maisha Yetu

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday 27 July 2018

MSANII NANDI KUNOGESHA MISS TANZANIA KANDA YA KASKAZINI KESHO ARUSHA


Na Pamela Mollel,Arusha

Msanii Wa Mziki Wa kizazi kipya,Faustine Charles ,Nandy ameapa kufia jukwaani kesho wakati akitoa burudani ya kukata na shoka  na kukonga nyoyo za  wakazi Wa Jiji la Arusha katika shindano la kumsaka Miss Tanzania,kanda ya Kaskazini litakalofanyika katika.hotel ya Naura spring Kesho jumamosi ,Julai 28.

Nandy ambaye anatamba na wimbo wake Wa (Ninogeshe )ametangaza kutokuwa na mchumba na kuwataka wanaume mwenye uwezo Wa kumuoa ajitokeze kesho Naura hotel na yupo tayari kuolewa Arusha.

Shindano hilo la Miss Tanzania litashindaniwa na warembo 12 Wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ,ushindani unatarajiwa kuwa mkali kutokana na warembo wote kuwa wazuri.

Pia msaani huyo aliwataka wapenzi wa nyimbo zake kujitokeza kwa wingi ili waweze kufurahia burudani ambayo itakuwa ya aina yake

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here