Meneja Kiongozi wa Kampuni ya Monsanto Frank Wenga Akizungumza katika uzinduzi wa mbegu mpya aina ya DK 777 ,ulifanyika katika viwanja vya Kituo cha utafiti wa kilimo Selian jana Mkoani Arusha.Picha na Pamela Mollel Arusha
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Mbegu nchini Bob Shuma akizungumza katika uzinduzi wa mbegu mpya aina ya DK 777 jana Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa kilimo
Viongozi wa kampuni ya Monsanto na wadau wa kilimo wakiwa katika shamba darasa
Na Pamela Mollel,Arusha.
Kampuni ya Uzalishaji wa Mbegu ya Monsanto imezindua mbegu mpya aina ya DK 777 ambayo ina uwezo mkubwa wa kustahimili ugonjwa wa Mnyauko wa Mahindi uliowasumbua wakulima wengi hususan katika kanda ya Kaskazini na kusababisha wakulima kukosa mazao .
Mtafiti wa Mbegu hizo kutoka kampuni ya Monsanto ,Honest Temu amesema kuwa ugonjwa wa Mnyauko umeawaathiri wakulima wengi suala lililowasukuma kufanya utafiti ambao ulikamilika hivi karibuni na mbegu hizo zilisajiliwa na serikali kwa ajili ya kutumika na wakulima .
Meneja Kiongozi wa Kampuni hiyo Frank Wenga amesema kuwa mbegu hizo zitakua mkombozi kwa wakulima na kuleta mavuno ya kutosha kwa ajili ya chakula na ziada kwa ajili ya biashara ili kukuza pato la mkulima na kuinua uchumi wa taifa kupitia kilimo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Mbegu nchini Bob Shuma akizindua mbegu hizo amesema kuwa sekta ya mbegu ni sekta muhimu katika kukuza kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa taifa hivyo wadau wa mbegu hawana budi kufanya tafiti zitakazosaidia kukuza kilimo na kuinua ustawi wa mkulima kupitia uzalishaji wa mbegu bora.
Kwa upande wake Mkulima Nko amesema kuwa mbegu hizo zitawasadia wakulima kupata uhakika wa kupata mazao ya kutosha kutosheleza mahitaji ya nyumbani na mahitaji ya soko hivyo kusaidia upatikanaji wa chakula na kukuza pato la mkulima
No comments:
Post a Comment