Kamishna wa Bima nchini , Dkt. Baghayo A. Saqware akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo mara baada ya kuzindua mfumo wa kieletroniki ujulikanayo kama Tanzania Imports Insurance Portal(TIIP)utakao wezesha waagizaji bidhaa nje ya nchi kununua Bima toka kampuni za kitanzania,mfumo huo umeandaliwa na TIRA ikishirikiana na Taasisi ya Bima nchini (IIT)warsha iliyofanyika juzi jijini Arusha na kuhudhuriwa na wadau wa Bima.(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)
Meneja wa kanda kaskazini wa usimamizi mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Elieza Rweikiza akizungumza katika mafunzo hayo jijini Arusha Juzi
Wadau wa Bima wakisikiliza kwa makini
Mkurugenzi wa Leseni na Usimamizi wa Mwenendo wa Soko Samwel Mwiru akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ambapo pamojana mambo mengine alisema kuwa Soko la bima Tanzania linaendeshwa na kampuni za bima zipatazo 31,madalali takribani 150 na wakala wa bima wapatao 413,Sekta ya bima husimamiwa na Mamlaka ya usimamizi wa bima (TIRA)kwa mujibu wa sheria ya bima ya mwaka 2009
Rais wa Taasisi ya Bima Tanzania BoscoJames Bugali akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha
Meza mkuu
Mkurugenzi wa Leseni na Usimamizi wa Mwenendo wa Soko Samwel Mwiru(kushoto)akiwa na Mkurugenzi wa sheria TIRA
Meneja wa kampuni ya Bima ya Britam Lois Yateru akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo
No comments:
Post a Comment