Katibu Mkuu Wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga
Taifa Florens Turuka akisalimia na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddy Kimanta
Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania Jenerali Vanance Mabeyo akisalimiana na Kaimu Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha Dokt Faraji Kasidi, katikati ni Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA), Dokta Paul Massao
Katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga
Taifa Florens Turuka akisalimia Generali Maj Othaman
mara ya
kuwasili katika chuo cha mafunzo ya kijeshi Mondoli(TMA) kwa ajili ya uzinduzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo
Katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa Florens Turuka akisalimiana na Dr. Adolf B. Rutayuga ambaye ni kaimu mtendaji mkuu wa NACTE.
Katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa Florens Turuka akizungumza katika uzinduzi wa uzinduzi wa shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo
Mkuu wa majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akitoa hotuba fupi katika halfa ya uzinduzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo
Meja jenerali Paul Peter Masao ambaye ni mkuu wa chuo cha mafunzo ya maafisa wanafunzi jeshi la ulinzi la Tanzania(TMA).
Kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema mahusiano kati yao na chuo hicho cha kijeshi yameanza muda mrefu ambapo wao
wamekuwa wakifundisha askari hao mafunzo ya kiraia.
kushoto aliyevalia suti ni Profesa Johannes Monyoambaye aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha(IAA)
Wanafunzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo leo
Maafisa wa jeshi wakitumbuiza wata wa uzinduzi wa wafunzo ya sayansi ya kijeshi.
Picha ya pamoja
Na Pamela Mollel,Monduli
Katibu Mkuu wa wizara ya
ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dokta Florens Turuka amesema kuwa jeshi hilo
hivi sasa limejipanga katika kukabiliana na changamoto za ulinzi na usalama kwa
kuwapatia askari wake mafunzo maalumu ya sayansi ya kijeshi.
Aliyasema hayo Jana
wakati akizungumza katika uzinduzi wa shahada ya kwanza ya sayansi ya kijeshi
inayotekelezwa na chuo cha uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Chuo cha mafunzo
ya kijeshi Monduli (TMA).
Alisema kuwa, kumekuwepo
na matishio mengi ambayo yamekuwa yakijitokeza Kwa namna tofauti ambapo hivi
sasa matishio hayo yamegeuka na kuhamia kwenye mitandao, hivyo kama jeshi wana
wajibu wa kujipanga zaidi kwa kuwaandaa maaskari ili waweze kukabiliana na hali
hiyo mahali popote.
Dokta Turuka alisema
kuwa, wao Kama jeshi ni wajibu wao kujipanga mapema kwa kuangalia namna ya
kuwajengea uwezo hasa katika maswala ya sayansi na teknolojia ili kuboresha
ulinzi na usalama hapa nchini.
Kwa upande wa Mkuu wa
majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo alisema kuwa wamekuwa wakitoa mafunzo
hayo kwa maaskari wake kulingana na mabadiliko ya kidunia hasa katika maswala
ya sayansi na teknolojia kwani ni eneo ambalo linahitaji elimu kubwa
zaidi.
Alisema kuwa, ni lazima
wasonge mbele na kwenda na wakati kwani wasipofanya hivyo watabaki nyuma na
kamwe hawataweza kukabiliana na vitisho vilivyopo hivi sasa.
Naye Mkuu wa chuo cha
mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA), Dokta Paul Massao alisema kuwa, wamekuwa
wakitoa masomo ya kijeshi na kiraia ili kuwaandaa vijana katika hatua ya ngazi
za juu zaidi kielimu ambapo kwa kuanzia kozi hiyo watahiniwa
158 wataanza kozi hiyo mapema.
Kwa upande wa Kaimu mkuu
wa chuo cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi alisema kuwa, mahusiano kati
yao na chuo hicho cha kijeshi yameanza muda mrefu ambapo wao wamekuwa
wakifundisha askari hao mafunzo ya kiraia ambayo yamekuwa yakileta manufaa
makubwa Sana.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment