Makamu
wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan akiongea
wakati wa ufunguzi wa kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB) uliofanyika jijini Arusha leo(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
Waziri wa Fedha na mipango(Mb)Dkt Philip Mpango akizungumza katika kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.
Mwenyekiti wa bodi ya PSPTB Dkt.Hellen Bandiho akizungumza katika kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira akiwa katika kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.
Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo akiteta jambo na
Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan katika kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.
Wadau wa mkutano huo wakifatilia kwa ukaribu
Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.
Na Pamela Mollel,Arusha
Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya
fedha na mipango kuhakikisha wanakamilisha mapema sera yaTaifa ya Ununuzi wa
Umma kwa kufanya marekebisho ya sheria ,kanunina taratibu zingine zikakazo
ongoza shughuli za ununuzi wa umma hapa nchini
Akizungumza leo jijini Arusha katika kongamano la nane la wanataaluma ya ununuzi
na ugavi(PSPTB)iliyowashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wadau kutoka nchi
jirani ya Kenya
Bi.Samia alisema kuwa kwa kufanyika kwa marekebisho ya
sheria ya ununuzi wa umma utasaidia kuongeza kiwango cha uwajibikaji wa wadau
wote wanaohusika katika shughuli za umma
Aidha aliongeza kuwa ripoti mbalimbali za ukaguzi
zinaonyesha kuwa Serikali imeendelea kupata hasara katika eneo la ununuzi
wa umma kutokana na wataaluma wachache kutokuwa tayari kutimiza wajibu wao au
shughuli hizo kufanywa na watu wasio na taaluma hiyo
“Napenda kuwaasa ambao bado wanaendeleza vitendo viovu
kama rushwa ,upendeleo,wizi,uzembe waache mara moja na watambue kuwa sheria
zipo na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao”alisema Bi.Samia
Pia alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano haitamvumilia
mtu yeyote atakaye kwenda kinyume na maadili ya taaluma yake
Kwa upande wake Waziri wa Fedha na mipango(Mb)Dkt
Philip Mpango alibainisha mapungufu yaliyoonekana katika taasisi zilizokaguliwa
ikiwemo kupungua kwa kiwango cha uzingatiaji wa sheria ya ununuzi wa umma
katika Halmashauri kutoka wastani wa asilimia 71 mwaka 2015-16 hadi asilimia 69
Pia Mh.Mpangoalisema kuwa miradi 7iliyokaguliwa
yenyethamani ya shilingi bilioni 2.37 imebainika kufanywa chini ya
viwangovisivyoridhisha
Aidha aliongeza kuwa kwa upande wa maadili ya ukaguzi
umebaini kuwepo kwa viashiria vingi vya rushwa katika usimamiziwa miradi 33
katika taasisi 17 za Umma zilizokaguliwa hivi karibuni
Naye Mwenyekiti wa bodi ya PSPTB Dkt.Hellen Bandiho
alisema kuwa changamoto inayoikabili bodi hiyo kwa sasa ni pamoja na waajiri
kuajiri watumishi wa ununuzi na ugavi ambao hawajasajiliwa na bodi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment