BANC ABC YAANZISHA HUDUMA MPYA KWA WATEJA WAKE - JAMII BLOG

Jamii Yetu , Maisha Yetu

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday 3 December 2018

BANC ABC YAANZISHA HUDUMA MPYA KWA WATEJA WAKE


 Meneja wa Banc ABC Magabe Nyambuche akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha
Na Pamela Mollel,Arusha

Banc ABC katika kuwajali wateja wake wa maeneo mbalimbali hapa nchini imeanzisha huduma maalumu ya kutumia satellite ili kuwafikia kwa haraka zaidi

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha hivi karibuni, Meneja wa Benki hiyo Magabe Nyambuche alisema pamoja na kuboresha huduma za kibenki pia wameanzisha huduma hiyo ya satelite itakayokuwa na uwezo wa kuwafikia hata wateja wavijijini

Alitaja mikoa ambao kwa sasa wanatoa huduma hiyo ya satellite ni Arusha,Dar es salaam,Dododma na Mwanza

Alisema kuwa katika msimu huu wa sikukuu ya Chrismas wanatoa zawadi kwa wateja wote watakao weka pesa kwenye account(fixed account)watapata riba papo kwa papo


Pia aliwataka wananchi kujiunga na benki hiyo kwakuwa huduma zake ni nzuri 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here