MWANARIADHA Magdalena Shauri akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli
Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika
mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon yaliyofanyika juzi
wilayani hapo.(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
MWANARIADHA
Marco Joseph akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli
Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika
mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon yaliyofanyika juzi
wilayani hapo.
MWANARIADHA Asha Samwe akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli
Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika
mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya pili yaliyofanyika juzi
wilayani hapo.
MWANARIADHA Josephat Joshua akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli
Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika
mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya pili yaliyofanyika juzi
wilayani hapo
Mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli
Rebecca Lobulu akizungumza katika mashindano hayo mara baada ya kukabidhi zawadi washindi walioongoza katika mashindano ya riadha
Kikundi cha ngoma kabila maarufu la kimaasai kikitoa burudani katika mashindano hayo,
Mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba akitoa zawadi shilingi elfu ishirini kwa mama aliyeshiriki mashindano hayo ya riadha huku akiwasii wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki michezo
Mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba akiwa katika picha ya pamoja na watoto walioshiriki mashindano hayo,amabapo alidhamini Zawadi za watoto zenye thamani ya shilingi laki tatu
Na PamelaMollel,Monduli
Mashindano ya riadha maarufu kwa jina la Monduli Maasai Maradhon imekuwa kivutio kikubwa kwa wananachi waliojitokeza kuangalia shindano hilo lililowashirikisha wadau mbalimbali
Mashindano hayo ya riadha yaliyofanyika juzi yanatajwa kuwa mashindano ya kwanza kufanyika Monduli na kufanya washiriki mbalimbali walioshinda kujinyakulia zawadi
Wanariadha
Marco Joseph na Magdalena Shauri wamefanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika
mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon
Kwa
wanaume waliokimbia kilomita 21 Joseph Kutoka talenti alitumia Muda wa
saa 1:19:27 akifuatiwa na Josephat Joshua Kutoka Polisi kwa muda wa
1:05:54 huku nafasi ya tatu akishilia Fabiano Joseph kutoka JWTZ kwa
muda wa saa 1:06:13.
Kwa
wanawake Magdalena Shauri aliongoza kwa muda wa saa 1:19:27 akifuatiwa
na Asha Samwe kwa muda wa saa 1:20:16 huku nafasi ya tatu ikimwendea
Mayselina Mbua kwa muda wa 1:20:32.
Zaidi ya wanariadha 200 walishiriki mbio hizo za km 21,km 5 na km 2.5 ambazo ziliongozwa na mkuu wa wilaya Monduli Idd Kimanta ambapo washindi walikabidhiwa Zawadi za fedha na medali na tishirt.
Washindi
kwa kilomita 21 kwa wanaume na wanawake ,Mshindi wa kwanza Alipata
shilingi laki 500,000 na ,mshindi wa pili 300,000 na Mshindi wa tatu
200,000, Mshindi wa nne 150,000 na Mshindi wa Tano 100,000 pamoja na
katoni za vinywaji huku Zawadi za mbuzi mnyama zilitolewa kwa baadhi ya
washindi wengine.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli
Rebecca Lobulu aliwapongeza waandaaji na washiriki,huku akisistiza kuwa michezo ni fursa ya ajira na pia inaimarisha mwili
Alitoa wito kwa wazazi kuwahimiza wototo michezo na badala yake waache kubeza watoto wanaofanya vizuri katika michezo
Mmoja wa waandaaji wa Monduli Maasai
Marathon Meja Humphrey Nyuchi ambaye ni mkurugenzi mwenza alisema lengo la mashindano hayo kuibua fursa zilizopo katika eneo hilo pamoja na kuimarisha michezo
Alisema
ni Mara ya Kwanza mbio hizo zinazinduliwa na matarajio mbio hizo
zitakuwa endelevu kwa ila maana ya kuwa zitafanyika kila mwaka mwishoni
mwa mwezi Juni .
Naye
mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba ambaye
walidhamini Zawadi za watoto zenye thamani ya shilingi laki tatu alisema
kupitia michezo watotonwanaweza kufanya vizuri zaidi
Alisema
serikali iweke mkazo zaidi kuwekeza katika michezo kuanzia ngazi za
chini ili kuweza kuwa na vijana watakaofanya vizuri baadae na
kuliwakilisha taifa vyema.
Mwisho
No comments:
Post a Comment