SHULE ZA SEKONDARI HAPA NCHINI ZATAKIWA KUWAPA MBINU WANAFUNZI KUFIKIA NDOTO ZAO - JAMII BLOG

Jamii Yetu , Maisha Yetu

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday 22 October 2018

SHULE ZA SEKONDARI HAPA NCHINI ZATAKIWA KUWAPA MBINU WANAFUNZI KUFIKIA NDOTO ZAO

Na Rose Jackson,Arusha

Wito umetolewa kwa shule mbalimbali za sekondari hapa nchini kujiwekea utaratibu wa kuwafundisha wanafunzi mbinu mbalimbali za kuejiepusha na vizuizi vya kukatisha ndoto zao za baadae

Aidha kwa sasa wapo baadhi ya wanafunzi hasa wa sekondari ambao wanashindwa kufikia malengo yao kutokana na kutokuwa na elimu halisi ya vikwazo vya ndoto zao

Hayo yamebainishwa na mkuu wa shule ya sekondari ya unambwe bw Edwin kaaya wakati akiongea na wanafunzi, walezi,pamoja na wazazi kwenye maafali ya kidato cha nne yaliyofanyika shuleni hapo mapema jana

Kaaya alidai kuwa kwa sasa wapo wanafunzi.wanaoishia njiani bila kufika mahala ambapo wamepataka kutokana na mambo mbalimbali hivyo basi ipo haja ya wakuu wa shule kuweza kuwapa maarifa hayo

Aliongeza kuwa wakiwa na maarifa hayo wataweza kujiepusha na vikwazo hivyo ambavyo wakati mwingine vinaepukika kabisa

Kutokana na hilo Kaaya alidai kuwa tayari wao kama shule wanatelekeleza hilo kwanza kusisitiza nidhamu ya hali ya juu

"kauli mbiu yetu hapa shuleni ni nidhamu,mwanafunzi akishakuwa na nidhamu ni raisi sana kuweza kujiepusha na vikwazo vitakavyoweza kukatisha ndoto zao za juu"aliongeza
Alihitimisha kwa kusema kuwa elimu ni fursa ambayo inatakiwa ipewe kipaumbele kikubwa kwenye jamii

Hataivyo kwa upande wa wanafunzi waliohitimu walidai kuwa uongozi wa shule hiyo umewapa maarifa na mikakati mbalimbali ya kuweza kuepukana na vikwazo ambavyo vitakwamisha ndoto zao za hapo baadae

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here