Serikali imeshauriwa
kuangalia uwezekano wa kuanza kuwekeza kwa watoto hasa wanaoishi katika
mazingira Magumu ili kuepusha dhana ya kuwa na taifa lenye watoto
ombaomba.
Kauli hiyo aliitoa Mkuu
Wa Nchi wa Shirika la Compassion Nchini, Agnes's Hotay alipokuwa kwenye
Mahafali ya Nne ya kuondoka kwenye ufadhili Wa shirika hilo kwa watoto
waliokuwa wakilelewa kwenye Klasta ya USA River, wilayani Arumeru, Mkoa wa
Arusha baada ya kufikisha umri Wa Miaka 22 .
Hotay amesema kuwa ipo
haja kwa serikali kuunga mkono jitihada zinazoonyeshwa na Mashirika , taasisi
mbalimbali katika kuwahudumia watoto waliopo katika mazingira magumu kwa
kuwapatia elimu na ujuzi ili waweze kujiajiri ,jambo litakalosaidia kupunguza
namba ya vijana wasio na ajira .
Amesema shirika hilo hapa
nchini limeifikia mikoa 17 na linafanya kazi na makanisa wenza zaidi ya 400 na
linahudumia watoto zaidi ya 93,000 ikiwa lengo ni kuwaondoa watoto kwenye
umasikini na kuwajengea uwezo Wa kujitegemea,kujikinga na maradhi na kuwajenga
kiuchumi.
Alitoa rai kwa wahitimu
kuhakikisha wanakuwa waadilifu kwa kuzingatia yale mema yote waliofundishwa na
walimu wao.
Awali katika risala ya
wahitimu hao wapatao 78 walilishukuru shirika la Compassion kwa ufadhili huo
ambao umewasaidia kuwajenga kiroho,kuwapatia Elimu ya ujasiliamali na kutaka
makanisa mengine kuinga mfano huo utakao saidia kupunguza changamito za vijana.
Naye Mwenyekiti wa Klasta
ya USA River ,Saluni Kisangas amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na Makanisa
wenza limekuwa likiwahudumia watoto tangia wakiwa na umri mdogo wa
kuingia chekechea na punde wanapofikisha umri wa miaka 22 wanaamini umri huo
wanastahili kujitegemea.
Aidha amesema katika
Klasta ya USA River inayohudumia kata 4 ,tangia kuanzishwa kwa Klasta hiyo
mwaka 1999 ambapo wahitimu wengi wamenufaika na Mpango huo kwa kupata
ajira serikalini na baadhi yao kuchukuliwa na mashirika Mbalimbali.
Mkuu Wa Nchi wa Shirika la Compassion Nchini, Agnes's Hotay akizungumza katika Mahafali ya Nne ya kuondoka kwenye ufadhili Wa shirika hilo kwa watoto waliokuwa wakilelewa kwenye Klasta ya USA River, wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha
Wahitimu
No comments:
Post a Comment