MKUU WA WILAYA ARUSHA AIPONGEZA SHIRIKA LA FOUNDATION FOR TOMORROW KWA KUHAMASISHA ELIMU - JAMII BLOG

Jamii Yetu , Maisha Yetu

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday 10 July 2018

MKUU WA WILAYA ARUSHA AIPONGEZA SHIRIKA LA FOUNDATION FOR TOMORROW KWA KUHAMASISHA ELIMU

 
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro aipongeza Taasisi ya  Foundation For Tomorrow kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhamasisha maswala ya elimu katika Mkoa wa Arusha awataka wadau wengine kujitokeza kuiga mfano huo' aliyasema hayo juzi katika Juma la Elimu katika shule ya msingi Levolosi jijini hapa, ambapo Taasisi hiyo iliandaa Tuzo maalumu kwa mwalimu bora(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
Meneja wa programu ya mafunzo kwa walimu Noah Kayanda kutoka shirika la Foundation for Tomorrow akizungumza katika hafla hiyo ,iliyofanyika hivi karibuni katika shule ya Levolosi jijini hapa,ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa wameaanda Tuzo hiyo kwa shule za msingi jiji la Arusha na Meru kwa walimu 20

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya sombetini,Caroline Kiyoja cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Sinoni,Dorice Mhina cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow 


Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Levolosi,Elizabeth Minja cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Uhuru,Jane Mkomwa  cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Lucky Vicent Julius Saunyi  cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow


Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Daraja  mbili Leah Mshana  cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow


Waalimu kutoka shule za msingi jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya cheti pamoja na kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mmoja Tuzo hiyo maalumu iliandaliwa na shirika la Foundation For Tomorrow kwaajili ya waalimu waliobainika kufanya kazi zao kwa umahiri mkubwa

Na Pamela Mollel,Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro ameipongeza Taasisi ya  Foundation For Tomorrow kwa kazi nzuri wanayoifanya katika  kuhamasisha maswala ya elimu katika Mkoa wa Arusha .

 Aliyasema  hayo juzi katika Juma la Elimu katika shule ya msingi Levolosi jijini hapa ambapo alisema shirika hilo limekuwa bega kwa bega katika kuhamasisha maswala mbalimbali ya Elimu na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuiga mfano huo

 “Foundation for Tomorrow wamekuwa mstari wa mbele sana katika maswala ya elimu mfano mzuri leo wameanda Tuzo maalumu kwa mwalimu bora ambaye amekuwa akifanya kazi zake kwa umahiri mkubwa”alisema Daqarro

Kwa upande wake Meneja wa programu ya mafunzo kwa walimu Noah Kayanda kutoka shirika la Foundation for Tomorrow akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa lengo la Tuzo hiyo ni kutia hamasa miongoni mwa walimu waliobainika kufanya kazi zao kwa bidii na umahiri mkubwa

Alisema kuwa katika zoezi hilo la kumsaka mwalimu bora limezingatia vigezo vyote ikiwemo uwezo wa kuhamasisha ufikiri wa kina miongoni mwa wanafunzi,uwezo wa kutengeneza mazingira ya kushiriki na mazingira rafiki ya kujifunza,uvumbuzi na ubunifu katika swala zima la ufundishaji na utekelezaji wa mtaala

Kayanda aliongeza kuwa vigezo vingine ni pamoja na kujikita katika kusaidia watoto wenye changamoto za kujifunza pamoja na uzoefu wa kujifunza

Alisema kuwa katika Tuzo hiyo ya mwalimu bora kila mwalimu atapewa zawadi ya cheti pamoja na kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mmoja 

MWISHO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here