Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akisalimiana na
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Arusha alipowasili katika
viwanja vya Gereza Kuu Arusha katika ziara Maalum ya uzinduzi wa nyumba
za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha leo Agosti 28, 2017 ambapo
nyumba hizo zimejengwa hivi karibuni na Uongozi wa Jeshi hilo kwa
kutumia fedha iliyopatikana katika miradi ya Shirika la Magereza.
Kushoto kwa Waziri ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt.
Juma Malewa.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha, leo
Agosti 28, 2017(Wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
nchini Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) ni Mbunge wa Jimbo la
Arusha Mjini, Mhe. Gobless Lema.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo
mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kutoa hotuba fupi ya uzinduzi
wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akitoa hotuba mbele
ya Maofisa na askari wa Magereza Mkoani Arusha katika hafla ya uzinduzi
wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(katikati) akikagua
nyumba za askari Magereza zilizojengwa kwa kutumia fedha iliyopatikana
katika miradi ya Shirika la Magereza(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa
wa Arusha, Khamis Nkubasi.
Muonekano wa nyumba zilizozinduliwa za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.
Baadhi
ya Maafisa na Askari wa Magereza Mkoani Arusha waliohudhuria hafla ya
uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akimpongeza Mkuu
wa Magereza Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza,
Khamis Nkubasi mara baada ya uzinduzi wa nyumba hizo(katikati) ni Naibu
Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akisalimiana na
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo(kulia) alipomtembelea ofsini
kwake leo kabla ya uzinduzi rasmi wa nyumba za makazi ya askari wa
Gereza Kuu Arusha.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Maafisa na Askari ambao ni mafundi ujenzi waliojenga
nyumba hizo(waliosimama) mara baada ya hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo.
Wengine walioketi ni Kamishna Jenrerali wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa(wa tatu toka kushoto), wa pili kushoto ni Mbunge wa Jimbo la
Arusha Mjini, Mhe. Gobless Lema(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza).
No comments:
Post a Comment