Mkurugenzi mkuu wa mfuko Gepf , Daudi Msangi akizungumza leo na vyombo mbalimbali kuhusu, mkutano wa wadau wa mfuko huo ambao
utashirikisha wadau zaidi ya mia tatu kutoka maeneo mbalimbali hapa
nchini,,mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Naibu waziri wa fedha na mipango Ashatu kijaja kufungua
mkutano huo wa wadau wa mfuko wa mafao ya mstaafu (Gepf)
utakaofanyika may 25 jijini Arusha.
Mwenyekiti wa bodi Ya
wadhamini, Joyce shaidi akiongea na vyombo vya habari ambapo amesema kuwa, mfuko huo unatarajia kuwekeza
kiasi cha kiasi cha shs bilioni moja na milioni mia sita katika kiwanda
cha kutengeneza mashine cha Kilimanjaro machine tools kilichopo Mkoani
kilimanjaro Kwa ajili ya kujenga kinu kidogo cha kufua vyuma.
Meneja masoko, Edgar shumbusho amesema kuwa, mfuko huo unalenga zaidi
kutumia radio za jamii katika kuwafikishia wananchi wa vijijini elimu
ambapo wamepata mafanikio makubwa Sana kupitia mfumo huo.
Kushoto ni Meneja wa mfuko huo Mkoa wa Arusha,Clement Saning'o akifatia kwa ukaribu mkutano na waandishi wa habari
Meneja wa mfuko huo Magraret Mrina wa wilaya ya Ilala akijitambulisha kwa waandishi wa habari
Kulia ni Afisa masoko wa mfuko huo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Saalam akiteta jambo na Adam Hamza afisa masoko
Kushoto ni meneja kutoka mfuko huo Ramadhani Sossora kutoka Mbeya akifurahia jambo na mkurugenzi wa Key Media Arusha Sarah Keiya mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari
Meneja wa mfuko huo kutoka Mtwara Deogratias Kakoko akijitambulisha kwa waandishi wa habari
Naibu waziri wa fedha na mipango Ashatu kijaja anatarajiwa kufungua
mkutano wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya mstaafu (Gepf)
utakaofanyika may 25 jijini Arusha.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo, Daudi
Msangi amesema kuwa, mkutano huo utashirikisha wadau zaidi ya mia tatu
kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.
Amesema
kuwa,katika mkutano huo wanatarajia kujadili Mada mbalimbali ikiwemo
kutoa elimu kwa wanachama pamoja na kuwasilisha taarifa za utendaji Kwa
mwaka 2015/2016.
Msangi
ameongeza kuwa, ndani Ya siku hizo mbili za mkutano mbali na kujadili
taarifa za wanachama wanatarajia kutoa misaada wa mashuka Kwa watoto na
wanawake wajawazito katika hospital ya dareda iliyopo wilayani babati
Mkoani Manyara.
Hata
hivyo ameongeza kuwa, mfuko huo umekuwa ukitoa misaada Kwa kuangalia
mahitaji ya jamii popote nchini na kuweza kusaidia kulingana na mahitaji
hayo.
Mwenyekiti
wa bodi Ya wadhamini, Joyce shaidi amesema kuwa, mfuko huo unatarajia
kuwekeza kiasi cha kiasi cha shs bilioni moja na milioni mia sita katika
kiwanda cha kutengeneza mashine cha Kilimanjaro machine tools kilichopo
Mkoani kilimanjaro Kwa ajili ya kujenga kinu kidogo cha kufua vyuma.
Amesema
kuwa,uwepo wa kinu hicho utasaidia kuinua uzalishaji wa kiwanda hicho,
huku kwa sasa watawekeza kinu kidogo ambapo kwa baadaye wataendelea na
kuwekeza kinu kikubwa.
Kwa
upande wa meneja masoko, Edgar shumbusho amesema kuwa, mfuko huo
unalenga zaidi kutumia radio za jamii katika kuwafikishia wananchi wa
vijijini elimu ambapo wamepata mafanikio makubwa Sana kupitia mfumo
huo.
Ameongeza
kuwa, mfuko huo umekuwa ukitoa mafao mbalimbali ikiwemo fao la msaada
wa mazishi Kwa wanachama wake, na sambamba na kutoa elimu kwa watoto wa
wanachama.
Aidha kauli mbiu Ya mkutano huo ni hifadhi ya jamii kwa wote inawezekana katika uchumi wa viwanda.
No comments:
Post a Comment