Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewataka wananchi waliovamia
maeneo ya hifadhi nchini, kujiandaa kuondoka ndani ya miezi mitatu kabla ya
operesheni kuanza.
Akizungumza na waandishi wa
habari,Julai 19 katika eneo la hifadhi ya Jamii ya wanyamapori(WMA)
ya makao, wilayani Meatu, Dk Kigwangalla alisema wavamizi wa maeneo ya hifadhi
wengi wamekuwa wakijihusisha na matukio ya ujangili.
"utakula kijiji kina ardhi
kubwa, lakini wengine wanajenga hadi katika ndani ya eneo la mita 500 kutoka
mpaka wa hifadhi na hao mara nyingi ndio wanaingiza mifugo hifadhini usiku na
kufanya ujangili"alisema
Alisema maeneo mengi ya hifadhi
na mapori ya akiba nchini yamevamia na wananchi jambo ambalo serikali haiwezi
kukubali yaharibiwe ama kutumika kwa ujangili.
Waziri huyo, pia alitembelea
kambi ya kitalii ya TGTS na hoteli ya Mwiba na kushuhudia
vikosi vya kupambana na ujangili katika maeneo hayo ambavyo vipo yapo chini ya
taasisi Friedkin Conservation Fund na kueleza kuridhishwa na uwekezaji wa
taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Mwiba Holding,
Abdukaril Mohamed, alisema katika eneo la Mwiba wamewekeza sh 2.2 bilion na
hivi sasa wanaendelea na shughuli za uhifadhi na utalii.
"mheshimiwa Waziri katika
eneo hili, kampuni yetu inafanya utalii wa picha na kuna hoteli,tunafanyakazi
kwa amani na utulivu na vijijini vinavyotuzunguka"alisema
Mwenyekiti wa kijiji cha makao,
Anthony Philip, alimweleza Waziri Dk Kigwangalla kuwa, katika eneo hilo kuna
mahusiano mazuri baina ya vijiji na wawekezaji na vijiji vinapata mgao wa
fedha.
Alisema kijiji cha makao
kimekuwa kikipata zaidi ya sh 147 milioni kwa mwaka kutoka kwa mwekezaji na
vijiji vingine sita vimekuwa vikipata zaidi ya milioni 80,000 kila mwaka"alisema.
Akiwa katika pori la akiba la
Maswa,Meneja wa pori hilo, Lusato Masinde alisema pia wanauhusiano mzuri na
wawekezaji ambao licha ya kulipia ada za vitalu pia wamekuwa wakitoa msaada wa
huduma mbali mbali ikiwepo maji.
Hata hivyo, alisema katika pori
hilo changamoto kubwa ni uvamizi wa mifugo, uchache wa watumishi na upungufu wa
vitendea kazi.
Mwisho.
Waziri wa Maliasili na utalii,Dk Hamis Kigwangalla akipata maelezo juu ya hoteli ya kitalii ya Mwiba kutoka kwa meneja wa hoteli hiyo,Alina Redka jana baada ya kutembelea hoteli hiyo iliyopo hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Makao
Waziri wa Maliasili na utalii,Dk Hamis Kigwangalla akipata maelezo juu ya mipaka baina ya kijiji
cha Makao na eneo la hifadhi kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Mwiba holding's Abdulkadir Mohammed jana eneo la Makao
Waziri wa Maliasili na utalii,Dk Hamis Kigwangalla alipotembelea hoteli ya kitalii ya Mwiba iliyopo ndani ya hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Makao
No comments:
Post a Comment