Waziri Joyce Ndalichako akizungumza na mmoja wa washiriki katika banda
mojawapo la sacids akipata maelezo kuhusiana na banda hiyo. hivi karibuni Mkoani Arusha
Na Happy Lazaro,Arusha
Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa Tanzania bado
inakabiliwa na ukosefu wa wataalam wenye ujuzi mbalimbali kuanzia ngazi
ya juu ya kati na ya chini.
Profesa
Ndalichako aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa miradi mikubwa
miwili kwenye vituo viwili vya mahiri vya elimu ya ujuzi katika kazi
za uzalishaji.
Alisema
changamoto hiyo ya ukosefu wa wataalam hivi sasa ni vyema iangaliwe
zaidi kwa kushirikisha wataalam pamoja na watu wasio na utaalam ambao
wanauwezo wa kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali hususan sekta za
utafiti.
Alisema
miradi hiyo miwili ambayo ipo katika vipengele vitano imefandhiliwa na
Benki ya Dunia ambayo imetoa kiasi cha zaidi ya Sh, bilioni 245
Alisema
mradi huo utasaidia zaidi wasomi zaidi ya 4000 sanjari na kutoa nafasi
za mafunzo kwa vijana 1000 wa vyuo mbalimbali na vijana 15,000 kwenye
fani mbalimbali za ujuzi.
Alisema
mradi huo umegawanyika katika sehemu mbalimbali ikiwemo kilimo,
utalii,ujenzi, nishati na madini pamoja na teknolojia ya habari na
mawasiliano
Alisema
kupitia mradi huo anatarajia ujuzi na utaalam zaidi kwenye tafiti
mbalimbali ikiwemo nafasi za kuimarisha vyuo mbalimbali kama Chuo Kikuu
cha Kilimo (Sua) pamoja na Chuo cha Nelson Mandela ikiwemo uimarishaji
wa vyuo vya ufundi na vinginevyo.
"Mradi
huu hakuna senti hata moja itakayoliwa badala yake imarisheni tafiti
mbalimbali na kutoa fursa kwa wengine ili kuinua sekta ya uchumi kwa
ngazi zote kuanzia ngazi za chini hadi za juu "
Naye
Mkuu wa Chuo hicho cha Nelson Mandela, Profesa Karoli Njau alisema
mradi huo wa unafanyika kwenye vyuo vikuu viwili ambavyo ni Chuo Kikuu
cha Kilimo (Sua) na Chuo cha Nelson Mandela.
Alisema
vyuo hivyo viwili vimebahatika kupata ufadhili huo baada ya kuandika
mchanganuo ulioshawishi benki ya dunia kutoa hela na kusisitiza kuwa
fedha hizo zilizotolewa zitatekelezwa katika malengo yaliyokusudiwa ili
kuleta tija pamoja na kutoa fursa kwa vijana kwa lengo la kuendana na
soko la ajira pamoja na fursa za kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya
viwanda.
Naye
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi na
Somalia, Bella Bird alisema benki hiyo imetoa fedha hizo kwaajili ya
kuwezesha tafiti mbalimbali vyuoni zitakazoleta matokeo chanya katika
sekta ya viwanda na uchumi
Alisema
Benki hiyo itaendelea kutoa ufadhili kwa vyuo mbalimbali pamoja ana
taasisi za sekta binafsi ili kuhakikisha vijana wanajikwamua kiuchumi na
kuondokana na umaskini kwa kubuni vitu mbalimbali ikiwemo tafiti zenye
tija kwa manufaa ya nchi pamoja na familia zao.
Mwisho
No comments:
Post a Comment