Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Bi.Jennista Mhagama akizungumza katika mkutano mkuu wa9 wa wadau wa mfuko wa hifadhi ya watumishi wa serikali za mita,LAPF jijini Arusha
Mkurugenzi wa KeyMedia Agency ya jijini Arusha akiwa katikati Bi.Barbra Keiya wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa LAPF, kampuni hiyo ilibeba jukumu la kualika vyombo vya habari kwaajili ya mkutano huo
Wakurugenzi wa KeyMedia Agency ya jijini Arusha Bi.Anna na Barbra wakiwa katika picha ya pamoja na mameneja wa LAPF
Baadhi ya wafanyakazi wa KeyMedia Agency ya jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja
Na Pamela Mollel,Arusha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Bi.Jennista Mhagama amewataka vijana kujiepusha na madawa ya kulevya ili utekelezaji wa dhana ya Tanzania ya viwanda ilete ajira kwa vijana wenye nguvu
Aliyasema hayo jijini Arusha wakati akifunga mkutano mkuu wa9 wa wadau wa mfuko wa hifadhi ya watumishi wa serikali za mita,
LAPF uliohudhuriwa na wadau wa mfuko huo
Alisema kuwa kwa sasa serikali imedhamiria kuwainua idadi kubwa ya vijana waliona ujuzu mdogo kwa kuwajenge uwezo kupitia mafunzo mbalimbali katika vyuo vilivyopo nchini
''Udhibiti mkubwa wa madawa ya kulevya unahitajika kwa vijana wetu ili kutengeneza taifa lenye nguvu ya kufanya kazi ''alisema
Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya watanzania hawana ujuzi wa kutosha hivyo basi serikali ya awamu ya 5 imejipanga ipasavyo kuhakikisha vijana wanapata ajira kupitia viwanda
Hata hivyo aliipongeza mfuko wa LAPF kwa kazi nzuri wanayofanya huku akiitaka mifuko yote ya kijamii hapa nchini ihakikishe kuwa ifikapo 2025 inakuwa na wanachama wengi zaidi.
No comments:
Post a Comment