Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto)
akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Utalii, Mhandisi atashasta Ndetiye kwa ajili ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan hususan eneo lenye mgogoro wa ardhi baina
ya kitongoji cha Uvinje na Hifadhi hiyo wakati wa ziara ya kamati hiyo
wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao
wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa
kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la
hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi
Atashasta Ndetiye (wa tatu kushoto) akizungumza na wananchi wa Kitongoji
cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa ardhi
baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara
ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi
wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume
cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja
kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa
fidia.. Wengine pichani ni Naibu Waziri,Wizara ya Maliasili, Mhandisi Ramo Makani(wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga (kulia).
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kushoto)
akiongoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii
kutembelea eneo lenye mgogoro baina ya Kitongoji cha Uvinje na Hifadhi
ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye eneo hilo
wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani jana. Wananchi
wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume
cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja
kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa
fidia. Wengine
pichani ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa
nne kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga (wa
pili kushoto).
Wajumbe wa kamati hiyo wakijadili baadhi ya mambo waliyoyaona katika eneo hilo lenye mgogoro.
Mkurugenzi
wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mtango
Mtahiko ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo
akiwasilisha taarifa ya Shirika hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan jana
wilayani Bagamoyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga (kushoto) akizungumza
na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii
kuhusu mgogoro baina ya kitongoji cha Uvinje na Hifadhi ya Taifa ya
Saadan.
Wajumbe wa kamati wakikagua eneo hilo la mgogoro.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania
(TAWA),ambaye alikuwa Muhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Dkt.
James Wakibara (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara na
Utalii wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani
Nkuwi kandokando ya fukwe za Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara
ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wilayani
Bagamoyo jana.
Baadhi
ya maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika la Hifadhi za
Taifa Tanzania (TANAPA) wakitembelea fukwe za Hifadhi ya Taifa ya Saadan
wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Utalii wilayani Bagamoyo jana.
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Paschal
Shelutete (kushoto) na Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Utalii, Gerald Magiri wakitembelea fukwe za Hifadhi ya
Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye hifadhi hiyo jana.
Mwenyekiti
wa kitongoji cha Uvinje, Hussein Akida akitoa maoni yake kuhusu mgogoro
huo mbele ya kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii jana. Kulia ni
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuri
(katikati), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
Tanzania (TAWA), Dkt. James Wakibara (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya
Mipango Wizara hiyo, Dkt. Iddi Mfunda wakisikiliza maoni ya wananchi wa
kitongoji cha Uvinje katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wilayani Bagamoyo
jana.
Baadhi ya wananchi wa kitongoji hicho wakitoa maoni yao mbele ya kamati.
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa
Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye (kulia) akizungumza na wananchi wa
Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa
ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa
ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi hao ambao wameweka
makazi ndani ya hifadhi hiyo wametakiwa kuondoka katika kipindi cha
mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi ambapo watalipwa fidia. Nyuma yake kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye.
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa
Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wananchi wa
Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa
ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa
ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi
wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume
cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja
kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa
fidia. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye.
Nyumba
inayodaiwa kuwa ni ya muwekezaji anaeshikilia moja ya eneo katika
hifadhi ya taifa ya Saadan kwa madai kuwa alipimiwa eneo hilo na
Serikali. Taarifa zilitolewa ni kuwa eneo hilo lilipimwa kiholela bila
ya kufuata taratibu za kisheria. Hata hivyo licha ya muwekezaji huyo
kutoka nchini Botswana kukaa katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka tisa
ameonekana hajaendeleza eneo hilo kwa lengo lililokusidiwa.
NA HAMZA TEMBA – WMU
………………………………………………………………..
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na
Utalii imeunga mkono uamuzi uliofikiwa na kamati maalum iliyoundwa na Serikali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya kumaliza mgogoro wa ardhi baina ya Hifadhi ya
Taifa ya Saadan na wananchi wa kitongoji cha Uvinje walioanzisha makazi ya
kudumu ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan kinyume cha sheria.

Kamati hiyo iliyoundwa na wajumbe watatu ambao ni
Serikali ya Wilaya ya Bagamoyo, Uongozi wa Kitongoji cha Uvinje na Shirika la
Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Saadan ilifikia maazimio kuwa
wananchi wa kitongoji hicho walioanzisha makazi ndani hifadhi hiyo waondolewe
kwa utaratibu wa kulipwa fidia ili kumaliza mgogoro huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Wilayani
Bagamoyo, Mwenyekii wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii,
Mhandisi Atashasta Ndetiye alisema baada ya kutembelea eneo hilo wamejiridhisha
kuwa Kitongoji hicho cha Uvinje kimeanzishwa ndani ya eneo la hifadhi ambapo ni
kinyume cha sheria.

“Kiuhalisia tumeona kuna kitongoji ndani ya
hifadhi ya Taifa ya Saadan, tumewasikiliza wananchi, tumesikiliza upande wa
Serikali, kwa mujibu wa taratibu na sheria wale wananchi wanapaswa watoe
ushirikiano, tunaamini kuna taratibu za Kiserikali zinafanywa kuhakikisha wale
wananchi wanalipwa ili waondoke kwa usalama” alisema Ndetiye.

Aliongeza, “tumeona jinsi ambavyo baadhi ya
wananchi hawako tayari kulipwa, lakini nadhani wakieleweshwa vizuri wataelewa
kuwa ile ni hifadhi ya Taifa, na kama ni hifadhi ya Taifa basi inahusu maslahi
ya Taifa, hivyo kila mwananchi anatakiwa atoe ushirikiano ili angalao Serikali
ifanye uwekezaji wa kueleweka”

Ndetiye alisema kamati hiyo imeshaweka maazimio kwa
ajili ya kushauri Bunge ili liazimie ni nini kifanywe na Serikali kumaliza
mgogoro huo. Alisema, “Kwa udharura wake na kutokana na maelezo ya mkuu wa
Wilaya, kwa ujumla kamati inakubaliana nayo kwasababu ameeleza vitu ambavyo
tumeona vina tija zaidi kwa watanzania na tunaenda kulishauri Bunge na Serikali
haraka iwezekanavyo ili hatua ziweze kuchukuliwa kumaliza mgogoro huo”.

Awali akielezea kuhusu mgogoro huo Mkuu wa Wilaya
ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga alisema baada ya maazimio ya kamati iliyoundwa
na Serikali ya wilaya kumaliza mgogoro huo baadhi ya wananchi walikubali
maazimio yaliyowekwa ya kulipwa fidia huku wengine wakikaidi kuondoka akiwemo
muwekezaji aliyeshikilia sehemu ya eneo hilo kwa zaidi ya miaka tisa bila
kuwekeza mradi uliokusudiwa ambapo wamepewa kipindi cha mwezi mmoja waondoke
kwa hiari kabla ya nguvu kutumika kuwaondoa.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Uvinje, Hussein
Akida alisema kitongoji hicho kilianzishwa ndani ya kijiji cha Saadan katika
Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani zaidi ya miaka 100 iliyopita huku kikiwa na
ukubwa hekta 3,000 na mpaka sasa Kitongoji hicho kina wakazi wasiopungua
72. Aliiomba Serikali kutambua mipaka ya kitongoji hicho pamoja na kuwasogezea
wananchi huduma za kijamii.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii walitilia mashaka uwiano wa kimahesabu wa taarifa
hiyo na uhalisia ambapo walihoji iweje kitongoji chenye miaka mingi kiasi hicho
kiwe bado hakijapewa hati ya kuwa kijiji kamili pamoja na idadi ndogo ya
wananchi wasiongezeka ndani ya muda mrefu wa miaka zaidi ya 100 toka kuanzishwa
kwa Kitongoji hicho.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhandisi Ramo Makani alisema, mgogoro huo uko wazi na unapaswa
kumalizika mara moja kwa kuwa Serikali ya Wilaya kupitia kamati iliyoundwa
imeshafikia maazimio ya kuwaondoa wananchi walioanzisha makazi ndani ya eneo la
hifadhi kinyume cha Sheria. Alitoa wito kwa wananchi kutii sheria za hifadhi na
kuheshimu mipaka iliyowekwa kuepusha migogoro isiyo ya lazima baina ya Serikali
na wananchi.

No comments:
Post a Comment