SHIRIKA LA FOUNDATION FOR TOMORROW YATOA ZAWADI YA FEDHA MASHULENI - JAMII BLOG

Jamii Yetu , Maisha Yetu

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 5 September 2017

SHIRIKA LA FOUNDATION FOR TOMORROW YATOA ZAWADI YA FEDHA MASHULENI


Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Naura juzi jijini Arusha baada ya shirika hilo kudhamini shindano la kuwasaka wanafunzi bora katika masomo ya Sayansi,Hesabu na Mawasiliano

  Meneja Mafunzo ya stadi za Maisha Hilda Lema kutoka shirika la Foundation for Tomorrowa kulia akiwa katika picha ya pamoja mara baaada ya kumkabidhi mwanafunzi wa shule ya sekondari Arusha day zawadi ya fedha na cheti baada ya kuibuka mshindi katika shindano la kuwatafuta
wanafunzi bora katika masomo ya Sayansi,Hesabu na Mawasiliano


Mkuu wa wa shule ya Sekondari Lemara Mkoani Arusha Risala S. Juma akiwa katika picha ya pamoja na mwanafunzi wake wa kike kidato cha Nne shule ya Sekondari Lemara Victoria Kira aliyefanya vizuri katika somo la Sayansi



Afisa elimu Taaluma Sekondari jiji la Arusha Prosper Kessy wakati akizungumza kwa nyakati tofauti katika shule za Sekondari zilizopo katika jijili la Arusha zilizoshiriki katika shindano la kuwasaka wanafunzi bora katika masomo ya Sayansi,Hesabu na Mawasiliano lililokuwa likiendeshwa na shirika la Foundation for Tomorrow


Wanafunzi wa shule ya Sekondari Arusha day wakiwa wanafatilia kwa ukaribu





 Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari  Naura katika ni mwanafunzi aliyefa vizuri shuleni hapo akiwa na zawadi kulia ni
Meneja Mafunzo ya stadi za Maisha Hilda Lema kutoka shirika la Foundation for Tomorrowa

Kulia ni Makamu Mkuu wa shule ya Arusha Day Dionisia Mrosso akiwa anapokea cheti kutoka kwa
Meneja Mafunzo ya stadi za Maisha Hilda Lema kutoka shirika la Foundation for Tomorrowa







Na Pamela Mollel,Arusha

Wanafunzi hapa nchini wametakiwa kusoma kwa bidii wawapo mashule ili waweze kutimiza ndoto zao za baade huku wakishauriwa kutojiingiza katika makundi mabaya 

Rai hiyo ilitolewa juzi na Afisa elimu Taaluma Sekondari jiji la Arusha Prosper Kessy wakati akizungumza kwa nyakati tofauti katika shule za Sekondari zilizopo katika jijili la Arusha zilizoshiriki katika shindano la kuwasaka wanafunzi bora katika masomo ya Sayansi,Hesabu na Mawasiliano lililokuwa likiendeshwa na shirika la Foundation for Tomorrow

Kessy alisema kuwa lengo la wanafunzi hao kuwepo shuleni ni kusoma kwa bidii hali itakayowapelekea kufaulu vizuri masomo yao na ufaulu huo ni faraja kubwa kwa Serikali,wazazi pamoja na jamii

Kwa upande wake Meneja Mafunzo ya stadi za Maisha Hilda Lema kutoka shirika la Foundation for Tomorrow ambao ndio waaandaaji wa mashindano hayo alisema kuwa shindano hilo lilishirikisha shule 26 za Sekondari jiji la Arusha 

Alisema kuwa lengo la shindano hilo nikuwapa hamasa wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi,Hesabu na Weledi katika Mawasiliano (Insha) sanjari na kusaidia walimu kugundua pengo katika masomo hayo na kuongeza bidii

Aliongeza kuwa katika shindano hilo  walifanikiwa kuwapata washindi 
 watatu hesabu,washindi watatu Sayansi,washindi wawili Insha ya kingereza na wawili Insha ya Kiswahili hivyo jumla ya washindi kumi walijinyakulia zawadi za fedha

Alisema kuwa washindi wanne walipata shilingi 100,000,wanne 75,000 nawawili  50,000  na walimu wawili ambao walikuwa wakiwasaidia wanafunzi walioshinda katika masomo hayo waliweza kujinyakulia shilingi laki moja kila mmoja 

Kwa Upande wake mwanafunzi wa kike kidato cha Nne shule ya Sekondari Lemara Victoria Kira aliyefanya vizuri katika somo la Sayansi na kushika nafasi ya kwanza katika shindano hilo alisema siri ya ufaulu wake nikusoma kwa bidii

Kira alitoa pongezi kwa  shirika hilo kwa kuja na wazo la kuwashindanisha wanafunzi katika masomo hayo ambapo  shindano hilo linawapa hamasa wanafunzi na walimu shuleni

“ Ndoto yangu  kubwa nikuja kuwa Daktari bigwa hivyo nawashauri wanafunzi wenzangu  kutokukata tama katika masomo yao bali waongeze bidii”alisema Kira
Mwisho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here