Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo afungua barabara ya Mahakama – St. James wakati wa ziara yake Jijini hapa.
Jiwe la Msingi lililowekwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwenye barabara ya Mahakama – St. James
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo(Pili kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Jiji pamoja na
Katibu wa CCM Wilaya wakikagua barabara ya Oljoro – Kisimani(4Km)
iliyojengwa kwa kiwango cha Changarawe.
Kutoka Kulia ni Mhandisi wa
Majengo Samwel Mshuza akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo(Pili Kulia) ramani ya Kituo cha Afya Muriet kinachojengwa kwa
mapato ya ndani ya Halomashauri ya Jiji.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (mbele) akikagua ujenzi wa kituo cha Afya Muriet.
………………
Jiji la Arusha lina Mtandao wa
barabara zenye urefu wa Km 334 na kati ya hizo barabara za Lami ni Km
86.7 tu na zilizobakia ni Changarawe pamoja na barabara za udongo.
Tangu Halmashauri hii ilipopata hadhi ya kuwa Jiji imeanza kutekeleza
mkakati wa ujezi wa barabara za Lami kila mwaka wa Fedha kwa kutumia
mapato ya ndani.
Halkadhalika
Halmashauri imeendelea kutafta miradi kutoka Tamisemi na Mfuko barabara
ili kuongeza mtandao wa barabara za Lami pamoja na changarawe kufanya
mji huu kuendana na hadhi ya Jiji.
Mwaka wa Fedha 2016/2017
Halmashauri imeendelea na kazi ya uboreshaji wa miundombinu kwa kujenga
barabara za Lami atika Maeneo ya Mahakamani – Kaloleni (0.65Km), Unga
Ltd – Muriet (5.9 Km), Bp – Sunflag –Njiro (0.85) ambazo zote zimegharmu
zaidi Tsh Bil 7 kutoka Mapato ya ndani, Mfuko wa barabara pamoja na
Mradi wa Tscp.
Miradi yoyte ta barabara
imefunguliwa, kukaguliwa na kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo wakati wa ziara yake iyokamilika mwishoni mwa wiki
iliyopita ambapo pia aliweza kufungua barabara ya Oljoro Kisimani
iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe (4 Km) pamoja na Ujenzi wa Daraja
la Oljoro.
Kupitia ziara hiyo Mhe. Gambo
ameweza kufungua madarasa 17 kwa niaba ya madarasa 60 ya Shule za Msingi
yaliyojengwa, madarasa 7 kwa niaba ya madarasa 15 ya Sekondari na
kutembelea ujenzi wa vituo vya Afya 2 maeneo ya Muriet na Moshono
ambavyo vyote ujenzi wake umeanza kwa mwaka huu wa Fedha
No comments:
Post a Comment