Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kongwa, akisalimiana na Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Dodoma, Bi. Rehema Hamisi wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mifuko 200 ya Saruji iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya kusaidia Ujenzi wa Nyumba ya Walimu wa shule hiyo iliyopo jimboni kwake Kongwa mkoani wa Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai, akisalimiana na Meneja wa Kituo cha Huduma kwa Wateja Njia ya Simu (Call Center), Ena Mwangama, wakati alipowasili katika Shule yua Sekondari ya Laikala.
Spika wa Bunge, Job Ndugai na Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Dodoma, Rehema Hamisi wakielekea shuleni hapo.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tawi la Dodoma, Rehema Hamisi (wa pili kushoto), akipiga ngoma sambamba na wasanii wa kikundi cha Matumaini kilichokuwa kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi waBenki ya CRDB Tawi la Dodoma, Bi. Rehema Hamisi, akisoma hotuba katika hafla ya kukabidhi msaada wa mifuko 200 ya Saruji iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Kusaidia Ujenzi wa Nyumba ya Walimu katika Shule ya Sekondari Laikala.
Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambaye pia ni mbunge wa Kongwa, akipokea mfano wa hundi ya Sh. Milion 15 kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tawi laDodoma, Rehema Hamisi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya walimu katika Shule ya Sekondari Laikala iliyopo wilayani Kongwa. Kulia ni Diwani wa Kata ya Sagala, Simon Kamando, akishuhudia.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Dodoma pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.
Wanafunzi wakifurahia mfano wa hundi iliyotolewa na Benki ya CRDB.
Spika wa Bunge, Job Ndugai, akitoa shukrani zake kwa Benki ya CRDB baada ya kupokea mifuko 200 ya saruji pamoja na hundi ya Sh. Milioni 15.
No comments:
Post a Comment