Sekretariet ya jumuiya ya Afrika mashariki yapata hati chafu inayotokana na kushindwa kutoa mipangilio ya hesabu kwa wakati. Arusha - JAMII BLOG

Jamii Yetu , Maisha Yetu

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday 7 October 2018

Sekretariet ya jumuiya ya Afrika mashariki yapata hati chafu inayotokana na kushindwa kutoa mipangilio ya hesabu kwa wakati. Arusha

Na wankyo gati,arusha

Sekretarieti ya jumuiya ya Afrika mashariki inayoongozwa na Katibu mkuu
wa jumuiya hiyo Liberat Mfumukeko imepata hati chafu inayotokana na
kushindwa kutoa mipangilio ya hesabu kwa wakati
.
Akisoma taarifa ya kamati ya Fedha na Mipango ya Bunge la Afrika
mashariki(EALA) Dkt.Ngwaru Maghembe amesema kuwa ripoti yao na
uchunguzi imebaini kuwa hakuna upotevu wa fedha wa la madudu ya
matumizi mabaya ya fedha.

Amesema kuwa sababu kubwa waliyotoa ni uchache wa Rasilimali watu na
uchelewaji wa kuandaa taarifa za fedha kwa wakati na kutoaandaa
taarifa za kihasibu kutokana na uchache wa watumishi kutokana na kuwa
na safari nyingi za kijumuiya hivyo kushindwa kuwasilisha kwa wakati
ripoti zao.

“Uchache wa watumishi lilichangia kutoandaa kwa taarifa za kiuhasibu
jambo ambalo lililochangia kupata hati chafu utaona jumuiya ilipanga
mwaka  wa fedha 2016\17 kutumia fedha za kimarekani million 106 kwa
ajili ya kujiendesha na zilifanya kazi sawa licha ya wafadhili
kupunguza fedha”alisema Dkt.Maghembe.

Amesema kuwa Katibu mkuu wa jumuiya hiyo amechukuwa hatua kadhaa
katika suala zima la kubana matumizi ikiwemo kupunguza safari za nje
kwa watumishi wa jumuiya hiyo jambo ambalo limesaidia kuweza kuongeza
fedha katika miradi mbali mbali.

Amesema kuwa jumuiya hiyo imejipanga kujiendesha yenyewe bila kusubiri
fedha za wahisani ambazo wakati mwingine zimekuwa zikichelewa na hivyo
kushindwa kutimiza malengo kama ilivyokuwa mwaka wa fedha 2016\17
wafadhili walipunguza fedha.

Amesema jumuiya inaweza kujiendesha bila kusubiria fedha za wafadhili
kama tunaweza kutimiza malengo yetu ya kuhudumia wananchi wa jumuiya
hii tunazo rasilimali kubwa katika nchi wanachama.

“Na mnukuu Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania akilihutubia bunge
hili jijini Dodoma alisema kuwa jumuiya hiyo isiwe omba omba kwa
kungojea fedha kutoka kwa wahisani na badala yake wao wajipange
kujiendesha kwa kuandaa mipango ya maendeleo bila kutegemea fedha za
wahisani”
Mwisho…

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here