WAZIRI KIJAJI AWATAKA WAHITIMU CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KUJIEPUSHA NA RUSHWA - JAMII BLOG

Jamii Yetu , Maisha Yetu

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 3 December 2017

WAZIRI KIJAJI AWATAKA WAHITIMU CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KUJIEPUSHA NA RUSHWA

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza juzi katika mahafali ya Chuo cha Uhasibu Njiro Arusha ambapo pamoja na mambo mengine amewaonya wahitimu nchini kujiepusha na rushwa kwa kutaka utajiri wa haraka kuacha tabia hiyo kwani hawatabaki salama katika utawala huu. (Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
 Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha uhasibu Arusha Bi.Rukia Adam akisoma maelezo ya chuo cha Uhasibu Arusha katika mahafali chuoni hapo juzi

Mkuu wa kitivo cha uhandisi,mazingira na Computer Paul David Greening kutoka Uingereza akizungumza katika mahafali yao juzi katika Chuo cha Uhasibu NjiroArusha
Kushoto ni mgeni rasmi ambaye ni NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji akisoma maelezo mafupi ya chuo cha Uhasibu Njiro Arusha katika mahafli juzi chuoni hapo


 Wahitimu wakifatilia mahafali hayo kwa ukaribu zaidi
 Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja,wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro,Dk.Faraji Kasidi akiteta jambo Naibu  Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji katika mahafali chuoni hapo juzi


Wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi

Baadhi ya watumishi wa chuo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi juzi katika mahafali chuni hapo

Na Pamela Mollel,ARUSHA 
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji ametoa onyo kali kwa  wahitimu wa Uhasibu nchini kujiepusha na rushwa kwa kutaka utajiri wa haraka kuacha tabia hiyo kwani hawatabaki salama katika utawala huu. 

Akizungumza juzi  katika mahafali ya 19 katika Chuo cha Uhasibu Njiro Arusha, wakati akitunuku vyeti vya ngazi mbalimbali viiwemo vya Uhasibu kwa wahitimu 1324, Dk.Ashatu alisema baadhi ya wataalamu wa Uhasibu wanachangia kurudisha nyuma Maendeleo kwa tamaa zao.

Alisema ni vema watumie elimu waliopata kubuni ajira na pale watakaotoa ajira wafanye kwa weledi na uadilifu.

Alisema endapo wataalamu hao watabadilika na kuwa na uadilifu itawezesha Taifa kufanikisha ndoto yake ya kufikisha uchumi wa Viwanda kabla ya mwaka 2025.

Aidha alipongeza Chuo kuwa wabunifu wa kuongeza kozi kulingana na huhitaji wa jamii hadi kufikia 33 ikiwemo ya Shahada mpya ya Kijeshi ilioanza kutolewa mwaka huu.

Kuhusu ombi la ujenzi wa Hosteli na kumbi za Mihadhara, alisema serikali itazitatua kulingana na jinsi wanapopata fedha,japo alishauri uongozi wa Chuo kuhakikisha sekta  binafsi wanaona watawasaidiaje.

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro,Dk.Faraji Kasidi alisema mwaka huu wameadhimisha  Mahafali  ya 19 ya Chuo hicho na ya nane ya Chuo hicho Kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Coventry ya Uingereza.

Alishukuru serikali kwa kutoa mikopo kwa nusu ya wanachuo wa mwaka wa kwanza 2017 na kufanikisha ndoto kwa watoto maskini.

Mwisho 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here