SHIRIKA LA FOUNDATION FOR TOMORROW LATOA TUZO MAALUMU KWA WALIMU WALIOSHIRIKI KATIKA KINYANG’ANYIRO CHA KUWASAKA WALIMU BORA MKOA WA ARUSHA - PAMWASH BLOG

Jamii Yetu , Maisha Yetu

Sunday, 17 December 2017

demo-image

SHIRIKA LA FOUNDATION FOR TOMORROW LATOA TUZO MAALUMU KWA WALIMU WALIOSHIRIKI KATIKA KINYANG’ANYIRO CHA KUWASAKA WALIMU BORA MKOA WA ARUSHA

SAM_3196
Kushoto aliyevalia koti jeusi ni Mgeni rasmi Mariam Kimoso ambaye alimuakilisha mkurugenzi wa jiji la Arusha akimkabidhi mwalimu aliyefanya vizuri hivi karibuni katika kinyang’anyiro cha kuwasaka walimu bora lililoendeshwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Foundation For Tomorrow jijini Arusha,katikati ni diwani wa kata ya Themi jijini Arusha,Milance Kinabo, (CHADEMA),(Habari Picha na Pamela Mollel-Arusha)

SAM_3173
Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep, akizungumza katika hafla hiyo ambapo alisema kuwa lengo ni kuwawezesha walimu kupata mamlaka ambayo itawasaidia katika ufundishaji wa wanafunzi bila ubaguzi wowote katika kufufua maendelea ya elimu

SAM_3176
Mgeni rasmi Mariam Kimoso ambaye alimuakilisha mkurugenzi wa jiji la Arusha akizungumza katika hafla hiyo

SAM_3163

SAM_3174

Mjumbe wa bodi wa shirika la Foundation for Donacian Lyaruu akizungumza katika hafla hiyo

SAM_3152
Diwani wa kata ya Themi jijini Arusha,Milance Kinabo, (CHADEMA),akiteta jambo na Bi.Narja Roel
SAM_3189
SAM_3194
 Mwalimu Pius Edward kutoka shule ya msingi Sing’isi akipokea zawadi kwa mgeni rasmi


SAM_3205

SAM_3221
 Mkurugenzi wa Upendo  Friends Isabella Mwampamba alisema kuwa mwalimu anatakiwa kuheshimika kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakifanya hivyo ni muhimu sana kuwatia moyo

SAM_3223
Mwenyekiti wa wakuu wa shule jiji la Arusha Msendekwa Reginard akizungumza katika hafla hiyo

SAM_3233
 Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep,akimkabidhi zawadi ya T-shirt diwani kata ya Themi jijini Arusha Milance Kinabo

SAM_3247
  Mkurugenzi wa Upendo  Friends Isabella Mwampamba akiteta jambo na Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep 
SAM_3242
 Picha ya pamoja
Na Pamela Mollel,Arusha

Wadau mbalimbali wa elimu wametakiwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na taasisi ya Foundation for tomorrow katika harakati za kuwapa uwezo walimu pamoja nakuwapa motisha hali ambayo itasaidia wanafunzi kufanya vizuri zaidi wawapo mashuleni

Akizungumza hivi karibu katika Tuzo maalumu ya walimu iliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Foundation For Tomorrow, Mgeni rasmi Mariam Kimoso ambaye alimuakilisha mkurugenzi wa jiji la Arusha,alisema kuwa walimu wanakazi kubwa sana hivyo ni vyema wakapongezwa kwa kazi nzuri wanayofanya

Alisema kuwa elimu kubwa inayotolewa na walimu kwa wanafunzi mashuleni itasaidia kuleta mandeleo na jamiii nzima itafaidika kupitia elimu hiyo

Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep, alisema kuwa lengo ni kuwawezesha walimu kupata mamlaka ambayo itawasaidia katika ufundishaji wa wanafunzi bila ubaguzi wowote katika kufukia maendelea ya elimu

“Mamlaka hayo ni kusimamia mitahala vyema huku walimu ambayo watakaoweza kufanya hivyo kuwapongeza ili wawezekufundisha wanafunzi vyema katika kufikia malengo endelevu kwa wanafunzi”alisema Melissa

Aidha alisema kuwa shirika hilo linalenga katika kuwapa wanafunzi uwezo wa kuchochoea na kuchambua mawazo wawapo mashuleni,kuwasaidia wanafunzi wanaohitahi kujifunza zaidi,

Kwa upande wake mkurugenzi wa Upendo  Friends Isabella Mwampamba alisema kuwa mwalimu anatakiwa kuheshimika kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakifanya hivyo ni muhimu sana kuwatia moyo


No comments:

Post a Comment