Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akiongea na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro jana wakati wa ziara yake ya kikazi ambapo aliwataka watumishi
wawe na utamaduni wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo akieleza umuhimu wa filam
katika kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ukumla wakati wa
kikao na Maafisa Utamaduni na watendaji wa Mkoa wa Morogoro.
Wajumbe
wa kikao wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (Hayupo pichani) wakati wa ziara yake
ya kikazi jana mkoani Morogoro.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akiongea na baadhi ya Wazee wa kimila wa Mkoa wa Morogoro wakati
wa ziara yake ya kikazi jana Mkoani hapo.
Baadhi
ya wazee wa kimila wa Mkoani Morogoro wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
(Hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi jana mkoani hapo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (Kulia) akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo
(SUA), Utawala na Fedha Dkt. Yonika Ngaga (kushoto) alipotembelea
makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini yaliyopo Mazimbu
Morogoro wakati wa ziara yake ya kazi jana mkoani hapo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa fundi bombo Idara ya
Matengenezo Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Bw. Ally Mkopi
alipotembelea makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini yaliyopo
Mazimbu mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kazi jana mkoani hapo.
(Picha na Lorietha Laurence –WHUSM).
No comments:
Post a Comment