MAGIGE FOUNDATION YATOA MSAADA DODOMA - JAMII BLOG

Jamii Yetu , Maisha Yetu

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday 23 April 2013

MAGIGE FOUNDATION YATOA MSAADA DODOMA





Asasi ya Kijamii ya Catherine Foundation jana imetembelea kituo cha kulelea wa watoto cha Matumaini Village kilichopo mkoani Dodoma ambapo walikwenda kutoa misaada mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi wa Asasi hiyo, Catherine Magige.
Katika Hafla hiyo Mgeni Rasmi alikuwa Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda ambapo asasi hiyo ilitoa vitu mbalimbali vikiwemo, Madaftari, Mafuta, Sabuni, Juice, miswaki na dawa zake, mchele, sukari, nguo za watoto, kanga za wakinadada wanaowalea watoto hao na vingine vingi.

Mama Tunu Pinda akihutubia

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akihutubia katika hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige akihutubia katika hafla hiyo

Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Catherine Magige akizungumza na watoto wanaolelewa kwenye Kito cha Matumaini Village kilichopo Dodoma alipokwenda kutoa msaada

Mhe Catherine Magige akicheza na mmoja wa watoto wa kituo hicho

Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige akiwa na mtoto mchanga anaye lelewa katika Kituo cha Matumaini Village mjini Dodoma jana.

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige wakizungumza na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.

Mama Tunu Pinda na Mhe Catherine Magige wakiwa na watoto hao

Mama Tunu Pinda akikabidhi zawadi mbalimbali zilizotolewa na asasi hiyo

Misaada mbalimbali ikitolewa

Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Catherine Magige akizungumza na watoto wanaolelewa kwenye Kito cha Matumaini Village kilichopo Dodoma alipokwenda kutoa msaada

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here