SERIKALI HAITAWAFUMBIAMACHO WEZI WA KAZI ZA SANAA:DKT MWAKYEMBE - JAMII BLOG

Jamii Yetu , Maisha Yetu

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 3 December 2017

SERIKALI HAITAWAFUMBIAMACHO WEZI WA KAZI ZA SANAA:DKT MWAKYEMBE

PIX 1 A
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akikata utepe leo Jijini Dar es Salaam kuashiria ufunguzi wa Kampuni  ya  Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji  wa kazi za Filamu hapa nchini.
PIX 1B
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akikata utepe leo Jijini Dar es Salaam kuashiria ufunguzi wa Kampuni  ya  Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji  wa kazi za Filamu hapa nchini.
PIX 2
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Tyeeo Entartainment Bw.John Kalaghe wakati wa  ufunguzi wa Mradi wa Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji  wa kazi za Filamu hapa nchini uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fissoo.
PIX 3
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi.Joyce Fissoo akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini.
PIX 4
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza  leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji  wa kazi za Filamu hapa nchini.
PIX 5
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati)  na viongozi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment wakionyesha Filamu ya “Queen of Masai”itakayoanza kusambazwa na Kampuni hiyo  kuanzia kesho. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
…………………………………………………………………………………………
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Serikali imesema itaendelea kuwachukulia hatua  wote watakaobainika kusambaza kazi za sanaa kinyume na utaratibu ili kuondoa kero ya muda mrefu ya wizi wa kazi za Sanaa uliolalamikiwa na wasanii wote hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akizindua Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment itakayohusika na usambazaji wa kazi za Sanaa kuanzia kesho.
“Serikali haitaendelea kuwafumbia macho wezi wa kazi za Sanaa,tutawashughulikia kama ambavyo tumeanza na mafanikio yameanza kuonekana yeyote anaetaka kusambaza kazi hizi aende Barazani Entartainment watamsaidia.”Alisema Dkt Mwakyembe.
Aidha amewataka wasanii wote hapa nchini kutumia Kampuni  hiyo kwa manufaa ili waweze kupiga hatua ambapo pia amewahakikishia kuwa ndani ya kipindi kifupi kijacho sekta ya Sanaa itakuwa na mageuzi makubwa.
Kwa upande wake Katibu wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amewahakikishia wasanii hao kuwa Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Wilaya wapo tayari kushirikiana na Kampuni ya Barazani Entartainment katika kuleta mafanikio ya kazi zao.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw.John Kalaghe ameishukuru Serikali kwa ushirikiano ilioupatia kampuni hiyo tangu ilipoanzisha wazo hilo ambalo leo limefanikiwa na wasanii wataanza kunufaika na kazi zao kwani  Kapuni hiyo itasambaza kazi zao kwa urahisi na salama zaidi.
Kampuni ya Tyeeo Barazani Entartainment itakuwa ndio wakala wa kusambaza kazi za sanaa ikiwemo Filamu za nje na ndani,Muziki,masomo ya watoto,na makala za kielimu kupitia simu ya mkononi kwa mitandao yote kwa malipo nafuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here