Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO),
Masanja Kadogosa (wa pili kulia) akiongozwa na Meneja Mradi wa reli ya
Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi (kushoto) pamoja na
Meneja mradi huo kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya YAPI Merkezi
kutoka Uturuki, Abdullah Milk mara baada ya kufika eneo la Soga - Kibaha
jumamosi usiku kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi
usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali.
Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi akitoa ufafanuzi juu ya mradi.
Watanzania
waliopata nafasi ya kufanyakazi katika mradi wa reli ya Kisasa ya
Standard gauge wametakiwa kufanya kazi kwa uweledi na kuacha
ubabaishaji.
Ujumbe huo aliutoa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya
Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa wakati alipofanya ziara ya
kushtukiza usiku wa jumamosi katika kambi mbalimbali za mradi huo
zilizopo Pugu mpaka eneo la Soga Kibaha ili kuona endapo wakandarasi wa
mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba
wao na serikali.
Kadogosa alisema mradi huo unatakiwa kwenda kwa kasi na kukamilika
haraka hata kabla ya muda husika hivyo kila mtu atakayefanya kazi katika
mradi huo anakikishe anafanya kazi na sio ubabaishaji utakaopelekea
mradi huo kuchelewa.
Aidha Kadogosa alisema wamefikia makubaliano ya kufanya kazi usiku na
mchana ili kuharakisha mradii huo na wakandarasi wanafanya haraka na kwa
ukubwa wa mradi huu ni lazima tufanye kazi usiku na mchana.
“Kama mnakumbuka wakati Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Makame
Mbarawa alipokuja hapa alisema ni lazima twende kasi na wakandarasi wetu
wameamua kwenda na kasi na sasa mnaona tuta linaendelea vizuri ni
lazima mradi huu ufanywe usiku na mchana kutokana na ukubwa
wake,”alisema.
Msafara huo ulipofika eneo la mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge Soga - Pwani.
Shughuli ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge Soga - Pwani ikiendelea.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO),
Masanja Kadogosa (wa kwanza kulia) akiongea machache na makandarasi wa
mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge wakati alipofanya ziara ya
kushtukiza katika kambi mbalimbali za mradi huo zilizopo Pugu mpaka eneo
la Soga -Kibaha ili kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya
kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali.
Meneja
Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi
akitoa ufafanuzi juu ya mradi.
Kwa upande wake Meneja Mradi huo kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi alisema kazi
inayoendelea kwa sasa ni kuendelea kusawazisha tuta ikiwa ni pamoja na
kukata na kujaza, kujenga mifereji na madaraja ya reli pamoja na kuweka
miundombinu ya umeme pamoja na vifaa vya kuongozea reli.
“Kazi imeanzia kilometa sifuri kutoka Dar es Salaam kwa sasa hivi
wakandarasi wanaendelea kazi ya tuta kukata na kujaza wana mitambo zaidi
ya 106 na kazi kubwa ni kujenga tuta wanaendelea vizuri ili kuhakikisha
wanakwenda kwa kasi inayotakiwa,”alisema Magedzi.
Kwa
upande wake Meneja mradi kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya YAPI
Merkezi kutoka Uturuki, Abdullah Milk alisema kampuni hiyo imejipanga
kuhakikisha mradi huo unatekelezwa usiku na mchana ili kuhakikisha mradi
unakamilika kwa wakati.
No comments:
Post a Comment