MKUU wa wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Fabian Daqarro, amemugiza afisa Usitawi wa Jamii wa halmashauri ya jiji la Arusha kuhakikisha wazee wote wa jiji hilo wanapatiwa vitambulisho kabla ya mwisho wa mwaka huu ili waweze kupata huduma mbalimbali ikiwemo matibabu mahospitalini.
Mhe. Daqaro ametoa agizo hilo kwenye mkutano na wazee wa jiji la Arusha uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa (AICC), ulikuwa una lengo la kusikiliza kero zao ili zipatiwe ufumbuzi na pia kufahamiana.
Mkuu huyo wa wilaya ameiagiza Idara hiyo kuhakikisha vitambulisho vinapatikana kabla ya mwisho wa mwezi ujao, sanjari na kuwataka watendaji wa serikali, mashirika ya umma na taasisi mbali mbali za serikali katika jiji la Arusha kuhakikisha kuwa zinatoa kipaumbele kwa wazee ambao wamekuwa hawapati huduma zao kwa wakati.
Aidha amewataka wenyeviti wa mitaa,kata na tarafa kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha wanaimarisha usalama kwenye maeneo yao ili kuwezesha wazee kuishi kwa usalama bila kubughudhiwa na kuhakikisha wanasimamia maadili.
‘’Mumepewa madaraka ya kuimarisha ulinzi. Yatumieni ili wazee wasibughudhiwe...Tambueni kuwa wazee ni watu muhimu na ndio waliotufikisha hapa. Sasa sitaki kusikia kuwa wanasumbuliwa... sitaki kusikia malalamiko ya kuporomoka kwa maadili ””alisema Daqarrro.
Wakichangia kwenye mkutano huo wazee wamedai kuwa taasisi za fedha pamoja na halmashauri ya jiji haziko tayari kuwakopesha wazee kwa hofu ya kuwa watakufa karibuni na kutaka dhana hiyo iondoke kwa kuwa kuzeeka sio kufa .
Wamesema nao wana mahitaji mbalimbali ya kuendesha sghuhuli zao za kiuchumi hivyo wanayo haki ya kupewa mikopo kama yalivyo makundi mengine ya jamii.
Wazee hao pia ameomba kushirikishwa kuanzia ngazi ya mtaa hadi halmashauri ili wawe na wawakilishi wao ambao watawasilisha kero zao kwenye vikao vya maamuzi vya serikali na baraza la madiwani. Pia wameomba wapate uwakilishi bungeni kama yalivyo makundi mengine ya walemavu, vijana na wanawake.
Wamelalamikia kukosa Vitambulisho ambavyo vingeliwawezesha kupata huduma za haraka kwenye taasisi mbalimbali za serikali,ikiwemo dawa kwenye hospital za serikali, pia wamelalamikia lugha za kuwadharirisha zinazotolewa na baadhi ya wahudumu wa hospital za serikali na vituo vya afya.Wamelalamikia hatua ya Zahanati kutokutoa huduma siku za mwisho wa wiki hali ambayo inawasababisha kukosa huduma za matibabu.Aidha wamelalamikia TASAF kutoa fedha kwa ajili ya watu wasiokuwa na uwezo kwa upendeleo ambapo walengwa wamekuwa hawanufaiki na mpango huo wa TASAF.
Katikati Ni mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha Bw. David Mwaiposa na kushoto ni mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya Arusha Mzee Mhina Sezua wakati wa mkutano na mkuu huyo wa wilaya kubaini changamto mbali mbali wanazokumbana nazo wazee wilayani hapa
Meza kuu wakifuatilia hoja mbali mbali zilizokuwa zinatolewa na wazee leo jijini Arusha
Sehemu ya wazee waliohudhuria mkutano huo wakiwa wanamsikiliza mkuu wa wilaya Gabriel Daqarro
Katibu wa wazee akiongea katika mkutano huo
WAALIMU WASTAAFU NAO HAWAKUWA NYUMA KWENYE KIKAO HICHO
Katibu Tawala wilaya ya Arusha David Mwaiposa akiwa anamkaribisha mkuu wa wilaya kuongea na wazee ilikujua kero zinazowakabili
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akiongea na wazee wa jiji la Arusha ambao wamemuomba mkuu huyo kuwafikishia salamu zao kwa viongozi wakuu wa serikali akiwemo raisi dkta John Magufuli kuwa wakifika Arusha waweze kuonana na baraza la wazee kama wanavyoonana na wazee wa Dar es salaam
Mwakilishi wa OCD nae akijibu maswali ambali mbali kwa niaba ya mkuu wa polisi wilaya ya Arusha
Mwenyekiti wa baraza la Wazee wilaya ya Arusha mjini Mhina Sezue akiongea katika mkutano huo ambao aliiomba serikali wilayani hapa kuwapa uwakilishi wazee kwenye mabaraza ya serikali kuanzia ngazi ya kijiji kata hadi Taifa huku wakimuomba raisi kuwapa nafasi moja katika zile kumi za uwakilishi wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Hata sisi hatupo nyuma kama walivyokutwa na kamera wakiingia ndani ya ukumbi wa Simba kwenye kituo cha mikutano cha AICC Leo Jijini Arusha
WAZEE HAWA NAO WALIKUWEPO KATIKA KUTOA MICHANGO YAO YA MAWAZO KUBORESHA HUDUMA ZAO
wakifuatilia mkutano huo kwa umakini
Bibi akifuatilia mkutano huo wa mkuu wa wilaya ya Arusha na wazee wa jiji la Arusha leo jijini Arusha
Sehemu ya wakifuatilia mkutano huo
Mandari ya muitikio wa wazee kwenye mkutano huo wakiwa katika ukumbi wa simba hall
wazee wakifuatilia mkutano huo kwa umakini na kueleza kero mbali mbali kwa mkuu wa wilaya ya Arusha
WAALIMU WASTAAFU NAO HAWAKUWA NYUMA KAMA HAPA WAKIFUTILIA MKUTANO HUO. Picha zote na Mahmoud Ahmad,Arusha
No comments:
Post a Comment