Naibu Waziri wa
Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu
Mh.Anthony Mavunde jana alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi rasmi msimu
wa FURSA 2017 mkoani Arusha.
“Tumehutubia
sana,tumesema sana,tumejadili sana,tumepanga mipango sana,sasa ni wakati
wa kuachana na dhana hii na kutenda,kufanya, na sio kufanya tu bali
kufanya kweli” ..
Ni maneno alionena
kwa hisia kali Naibu Waziri Anthony Mavunde akizungumza na mamia ya
vijana na vikundi mbalimbali mkoani Arusha Tanzania katika muendelezo wa
msimu wa FURSA 2017.
Naibu Waziri Mavunde
aliwataka Vijana kuhakikisha wanatumia fursa ya Mifuko 19 ya Uwezeshwaji
Wananchi Kiuchumi kama sehemu ya kupatia mitaji ya shughuli mbalimbali
za kiuchumi na hivyo kisaidia kuondokana na masharti magumu ya Taasisi
za Fedha nyingi.
Aidha pia,
Aliwashukuru sana timu nzima ya Fursa chini ya muasisi ndg.Ruge Mutahaba
kwa kuzidi kuisaidia jamii ya kitanzania na serikali kwa ujumla wake
kufanikisha maendeleo ya nchi hii na kuonesha kwa vitendo dhana nzima ya
ushirikishwaji.
Mgeni Rasmi ndugu
Mavunde aliizungumzia dhana hii ya Fursa na kauli mbiu yake mwaka huu ya
Anzia Sokoni akiwataka vijana na watanzania wote wanaotaka kufanikiwa
kutokata tamaa na kuwa na malengo yenye tija,kuhakikisha kila siku
wanaitumia kuwaza jambo la kufanya na la kuwaletea maendeleo.
Pia,alizungumza ni
namna gani serikali mpaka sasa imefanya katika kuhakikisha ina
watengenezea vijana mazingira bora na kukazania kwenye mipango iliyopo
kwao kuanzia wale walio katika mfumo rasmi wa elimu na wale walionje ya
mfumo kuwatengenezea mazingira ya kuendeleza shughuli zao mfano
useremala,ushonaji nk kuwapa mafunzo na kuwatengeneza kua bora.
Mwisho aliwashukuru
washriki wa Fursa 2017 Umoja wa mataifa kwa kuendelea kushika ajenda hii
ya vijana ikiwa kwa mkoa wa Arusha kupitia ILO wanaendelea kutoa
mafunzo ya uanagenzi kwa vijana,pia Letshego Tanzania kwa kujidhatiti
kuwasaidia vijana kwa mikopo na sapoti nafuu pia ushauri katika safari
yao ya kujikwamua kimaisha,wadau wengine ni wazara ya Afya na kampeni
yao ya NIPO TAYARI wakihimiza usafi hasa wa maliwatoni kunawa mikono.
Kuelekea kuhitimisha
Mh Mavunde alikubaliana na mtazamo wa FURSA 2017 wa Anzia Sokoni
akithibitisha kua katika lolote lile lazima kujua soko linataka nini.
No comments:
Post a Comment