Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Halmashauri ya
Mji wa Babati Bw,Daniel Luther wakati akiongea na waandishi wa habari katika maonesho
ya kilimo na mifugo Nane nane yenye kauli mbiu Zalisha kwa tija,mazao na bidhaa
za kilimo,mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ambapo kwa kanda ya
Kaskazini yanafanyika mkoani Arusha.(Picha na Pamela Mollel)
Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Halmashauri ya
Mji wa Babati Bw,Daniel Luther wakati akiongea na wananchi hili katika maonesho
ya kilimo na mifugo Nane nane yenye kauli mbiu Zalisha kwa tija,mazao na bidhaa
za kilimo,mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ambapo kwa kanda ya
Kaskazini yanafanyika mkoani Arusha.
Wananchi wakiwa wanaangalia bwawa la
samaki katika banda la halmashauri ya mji wa Babati katika maonyesho ya nane
nane
WATANZANIA wameshauriwa kutumia
teknolojia za kisasa katika kada za kilimo,mifugo na uvuvi ili kujipatia ajira
na kipato na hatimaye kukuza lengo la uchumi wa viwanda.
Ushauri huo ulitolewa jana jijini
Arusha na Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Halmashauri ya
Mji wa Babati Bw,Daniel Luther wakati akiongea na gazeti hili kwenye maonesho
ya kilimo na mifugo Nane nane yenye kauli mbiu Zalisha kwa tija,mazao na bidhaa
za kilimo,mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ambapo kwa kanda ya
Kaskazini yanafanyika mkoani Arusha.
Luther alisema kuwa endapo
watanzania wataamua kuwekeza nguvu zao katika teknolojia hizo ikiwemo ufugaji
wa samaki wataweza kujiingizia kipato katika ngazi ya kaya kupitia samaki
watakazozalisha.
"Ufugaji wa samaki kisasa si
lazima uwe na eneo kubwa hata eneo dogo nyumbani kwako unaweza ukafuga ama hata
katika simtank,madyaba ama pipa ili mradi eneo hilo liwe na hewa pamoja na
usafi wa mazingira ya maji ya kuhifadhia samaki wako.....
"Mradi huu unawezesha ajira na
thamani ya utengenezaji wake ni ndogo sana ukizingatia na faida utakayoipata
baadae hivyo vijana wachangamkie hii fursa kuliko kusubiri ajira
serikalini"alisema Luther.
Aidha aliwataka watanzania kuwekeza
katika kilimo cha mazao yenye thamani ikiwemo kilimo cha uyoga, mbogamboga za
majani,matunda na mizizi kwa kusindika mazao hayo ili kuendeleza soko lake na
kujipatia kipato.
"Msimu wa mavuno mazao yanakuwa
mengi na mengine yanaweza kuharibika lakini yakiweza kuongezewa thamani kwa
kukaushwa hasa mbogamboga tunaweza kuendelea kuwa na soko hili na kujiongezea
kipato..........
"Mfano zao la uyoga linaweza
kuendelea kupatikana katika soko kwakuwa umekaushwa tofauti na ukiwa mbichi
kwani huaribika kwa haraka
No comments:
Post a Comment