Picha ikimuonyesha Mkandarasi
kutoka Kampuni ya Caberisa Co.Ltd Bernad Mgohamwende ambaye anajenga barabara
kwa kiwango cha changarawe yenye ukubwa wa kilomita 36 eneo la barabara ya
mbauda ,Osunyai Mkoani Arusha iko
katika hatua za mwisho kukabidhi (Picha na Pamela Mollel)
Wakandarasi nchini bado wanakabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo upitaji wamagari makubwa bila ya kuwa na
vipimo maalum ambapo hali hiyo imekuwa ikiharibu miundombinu ya barabara ambapo
wamekuwa wakitumia gharama kubwa ya kufanya marekebisho mbalimbali ya kabla ya
kukabidhi barabara hizo kwa Serikali.
Hayo yameelezwa leo na mmoja
wakandarasi kutoka Kampuni ya Caberisa Co.Ltd Bernad Mgohamwende am,bae anajenga
barabara kwa kiwango cha changalawe yenye ukubwa wa kilomita 36 eneo la
barabara ya mbauda ,Osunyai iko katika kiwango cha changarawe
ambapo yuko katika hatua za mwisho kukabidhi ambapo iko katika wilaya ya
Arusha,Mkoa wa Arusha.
ALiongeza kuwa katika kutekelezaji
wa kujenga barabara hizo ,Serikali itaweka utaratibu wa kupima magari hayo
itawasaidia kuweza kutunza barabara hizo na kuweza kutotumia gharama kubwa kwa
wakandarasi .
Kwani Serikali italazimika kutoa
pesa za mara kwa mara kuwalipa wakandarasi kwa ajili ya kufanya marekebisho
ambapo hali hiyo inawatia hasara Serikali na kuwa na matumizi mabaya ya pesa
hizo.
Hata hivyo ameitaka Serikali kuweza
kutenga maeneomaalumu ya kuweza kupatikana kwa madini ya udongo na mchanga ili
kuwezwsha wkandarsi kupata madini hayo kwa urahisi kwani hivi sasa wanapata
changamoto kubwa katika udongo huo..
Aliongeza kuwa hivi sasa wananunua
udongo huo kwa wananchi ambapo wamekuwa wakiwauzia kwa gharama kubwa hali
ambayo imekuwa ikiwagharimu pesa nyingi ukilinganisha na hali halisi..
Kwa upande wake meneja wa Tanroad
Mkoa wa Arusha Mhandisi John Edward Kalupale alisema kuwa kuhusu suala hilo la
upitaji wa magari makubwa katika barabara inayijengwa ya Mbauda Osunyai ambapo
alisema kuwa kisheria hawaruhusiwi kuweka mizani kutokana na kuwa na barabara
hiyo kutokuwa na lami. ambayo hivi sasa iko kiwango cha changalawe.
Aliongeza kuwa wasafirishaji ni
waharibifu lakini wapende nchi yao na kuwa makini katika kutumia barabara
zinzoboreshwa kwa viwango vyote kuanzia changarawe mpaka lami kwani maendeleo
yoyote yale yanaletwa na uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara zote.
Ambapo katika barabara hiyo ya
osunyai mbauda wamekuwa yakipita magari makubwa ambayo yanajaza michanga na
udongo kupita kiasi na pia wanachanganya watu na michanga hhiyo hali ambayo
imekuwa ikiharibu barabara hiyo badala yake amewataka madereva wawe wazalendo
katika kutumia barabara hizo ili kuweza kuleta manufaa zaidi kwa watumiaji wote
ili kuweza kuzitunza na kuepusha serikjali kuweza kutumia pesa nyingi katika
kujenga barabara hizo.
Mhandisi John alisema kuwa arusha
bado kunakabiliwa na changamoto kubwa ya ardhi lakini wanafata taratibu za
kuwezesha kupatikana kwa ardhi ilikuweza kuepuka kupata madini udongo pindi
wakandarasi hao wanapohitaji kupata malighafi ya kutekeleza miradi wanyopewa na
serikali.
Katika kuweza kupata ufumbuzi
wakudumu wapo katika hatua za awali ambapo upembuzio yakinifu wa kina
unaendelea katika mhandisi mshauri unaendelea.
Ambapo wanatarajia kuweka lami
kilomita 400 kuanzia barabara ya Arusha,osunyai .olkesimate mpaka dosidosi
Kongwa ili kuweza kumaliza changamoto mbalimbali zilizoko .
Kwa upande wake dereva wa daladala
kutoka mbauda mpaka Olkesimati Erasto Msuya alisema kuwa marekebisho hayo ya
barabara yasmewarahisishia sana katika kupeleka abiria hao katika maeneo hayo
kwa kabla ya marekebisho hayo walikuwa wanapata tabu na changamoto kubwa sana
katika kuweza kutumia na kupelekja abiria eneo hilo.
Anapongeza sana Serikali ya awamu ya
tano katika kujenga miundombinu ya barabara na kuboresha maeneo ya barabara
mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment