Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania
Bi,Agness Kijazi wakati akiongea na waandishi wa habari katika mkutano
wa shirika hilo utakaofanyika kwa siku tatu mkoani Arusha
Na Mwanaid Bundala,Arusha.
SHIRIKA la Hali
ya Hewa duniani limeuingiza Mlima Kilimanjaro katika nchi zenye milima
yenye barafu (tropicsmom) ambapo ni moja ya uratibu wa shirika hilo.
Hayo yalisemwa
jana mkoani Arusha na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania
Bi,Agness Kijazi wakati akiongea na waandishi wa habari katika mkutano
wa shirika hilo utakaofanyika siku tatu mkoani hapo.
Alisema kuwa
katika majadiliano yaliyofanywa na shirika hilo waliona ni vema Tanzania
ikaingizwa katika nchi hizo kupitia mlima Kilimanjaro kutokana na
barafu inayopatikana katika mlima huo.
"Katika program
ya hali ya hewa kupima maeneo yenye barafu tutafikia makubaliano ya
kuweka kituo katika mlima Kilimanjaro ambacho kitaingizwa kwenye hii
program na mtaalamu mmoja wa Tanzania kutoka Mamlaka ya hali ya hewa
ataingia katika utafiti kama mjumbe katika shirika hili ili kuangalia
maeneo yenye barafu pamoja na kufanya vipimo vya hali ya hewa
duniani"alisema Bi Kijazi.
Aliongeza kuwa
moja ya faida ya mlima huo kuingizwa katika nchi hizo ni pamoja na
kusaidia kufahamu sababu za kupungua kwa barafu katika mlima huo kupitia
utafiti wa kisayansi utakaofanywa na shirika hilo.
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aliwaomba viongozi wa serikali kutoa
ushirikiano kwa wataalamu hao watakaofanya utafiti katika mlima
Kilimanjaro ili kuwawezesha kufanya kazi yao kwa ufasaha kwakuwa suala
hilo litaleta manufaa kwa taifa na sio mtu mmoja mmoja.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment