Mwenge wa Uhuru ukipelekwa eneo la mradi wa maji katika Kijiji cha Bukundi wilayani Meatu kwa ajili ya kufungua mradi huo.
Na Stella Kalinga, Simiyu
MWENGE wa Uhuru umeanza mbio zake rasmi leo katika mkoa wa Simiyu ambapo utapitia jumla ya miradi 43 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 8,450,841,622/=. Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati akitoa salamu za Mkoa huo kwa Kiongozi wa kitaifa wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 , Ndg.AmourHamad Amour katika kijiji cha Bukundi wilaya ya Meatu ukitokea katika mkoa Singida.
Mtaka amesema kati ya fedha hizo shilingi 680,285,524 zinatokana na Nguvu za wananchi ,Serikali Kuu shilingi 4,524,439,388, Halmashauri Shilingi 352,000,875, Washirika wa Maendeleo Shilingi 635,559,935 na Sekta binafsi Shilingi 2,258,555,900/=
Amesema Mwenge wa Uhuru utafungua miradi 14, kuzindua 13, kutembelea na kuona miradi 16 katika sekta ya Elimu,Afya,Maji,Vijana na wanawake, Miundombinu ya barabara, Sekta ya Viwanda, Maliasili, Kilimo, Ushirika na Utawala bora.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe.Anthony Mtaka akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa moja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa leo katika Kijiji cha Bukundi wilayani Meatu.
Aidha, Mtaka amesema katika kutekeleza kwa vitendo ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu 2017 usemao “SHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YANCHI YETU”, Mkoa wa Simiyu umeweza kujipambanua katika utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja, Bidhaa Moja, Kiwanda Kimoja”
“Katika utekelezaji huu mkoa umefanikiwa kuanzisha kiwanda cha Chaki wilayani Maswa, Kiwanda cha Maziwa wilayani Meatu na Upembuzi yakinifu unaendelea mingine minne ambayo pia itatekelezwa katika Halmashauri zetu nyingine nne” Ameongeza katika miradi kuwa kukamilika kwa viwanda hivyo kutasaidia kutoa ajira kwa vijana wa mkoa wa Simiyu na mikoa jirani kutokana na kuwa malighafi zinazotumika na zitakazotumika katika viwanda hivyo zinazalishwa hapa nchini.
Naye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru , Ndg. Amour Hamad Amour akifungua jengo la upasuaji kwa wanawake wajawazito katika kituo cha Afya Bukundi wilayani Meatu mbali na kuipongeza wilaya hiyo kwa kujali afya za wananchi wake hususani wanawake wajawazito pia alitaka mradi huo utunzwe na uthaminiwe.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akitoa salamuza Mkoa wakati wa kupokea Mwenge waUhuru kutoka Mkoani Singida katika kijiji cha Bukundi Wilayani Meatu.
“Mradi huu ni mzuri na mimi nimefurahi kuona naanza kuzindua miongoni mwa miradi inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, hasa akinamama wajawazito hivyo basi nitoe wito kwa wanawake kutumia vizuri jengo hili badala ya kujifungulia majumbani hali inayoweza kuhatarisha afya zenu, vile vile mradi huu utunzwe na kuthaminiwa ili uendelee kutusaidia,”alisema.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa wilaya ya Meatu wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza miradi ambayo imewasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali katika huduma za jamii ikiwemo maji na afya kwa kuwa itawasaidia kupata huduma hizo karibu na kwa ubora unaotakiwa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, Ndg. Amour Hamad Amour akifungua mradi wa maji katika kijiji cha Bukundi wilayani Meatu.
“Wakina mama wengi walikuwa wanapoteza maisha kwa kujifungulia njiani , kwa kweli naishukuru sana serikali maana kuwepo kwa jengo la upasuaji lililozinduliwa leo na mwenge wa uhuru,kutatusaidia sana ” amesema Tatu Athumani
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, Ndg. Amour Hamad Amour akizungumza na wananchi wa Kata ya Bukundi baada ya kufungua Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya cha Bukundi wilayani Meatu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, Ndg. Amour Hamad Amour akiangalia sehemu inayoandaliwa kwa ajili ya kuzalisha bio-gas kwa ajili ya kupata nishati itakayotumika katika kiwanda cha maziwa wilayani Meatu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, Ndg. Amour Hamad Amour akifungua jengo la Kitega uchumi la Chama cha Kuweka na Kukopa cha Walimu wa Wilaya ya Meatu KINYAKI SACCOS.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, Ndg. Amour Hamad Amour akiangalia moja ya chupa ya maziwa yanayozalishwa katika kiwanda cha Meatu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, Ndg. Amour Hamad Amour akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa wananchama wa KINYAKI SACCOS baada ya kufungua jengo la kitega Uchumi la SACCOS hiyo leo Mjini Mwanhuzi Meatu.
Wasanii wa Ngoma ya Asili wakitoa burudani wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katia kijiji cha Bukundi Wilayani Meatu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, Ndg. Amour Hamad Amour akikata utepe kabla ya kufungua jengo la kitega uchumi la KINYAKI SACCOS mjini Mwanhuzi wilayani Meatu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, Ndg. Amour Hamad Amour akikabidhi hundi kwa .baadhi ya wananchama wa KINYAKI SACCOS mara tu baada ya kufungua jengo la Kitega Uchumi la SACCOS hiyo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, Ndg. Amour Hamad Amour akimtwisha mkazi wa Kijiji cha Bukundi ndoo ya maji mara baada ya kufungua mradi wa maji katika kijiji hicho leo.
No comments:
Post a Comment