Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo,
akizungumza jambo baada ya kupatiwa taarifa ya kuingia kwa wahamiaji
haramu 72, huko Bagamoyo
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, alhaj Majid Mwanga
akitolea ufafanuzi tatizo la wahamiaji haramu wilayani hapo. (picha na
Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
Jeshi la polisi limewakamata wahamiaji haramu 72 raia kutoka nchini Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Aidha katika kipindi cha miezi sita,wahamiaji haramu 411 kutoka maeneo mbalimbali,walikamatwa wilayani Bagamoyo.
Kamanda wa polisi
wilaya ya Bagamoyo Adam Maro, alimwambia mkuu wa mkoa wa Pwani, Evarist
Ndikilo, kwamba wahamiaji hao walikamatwa usiku wa kuamkia jana .
Alieleza wahamiaji
hao walikutwa wakiwa wametelekezwa na mwenyeji wao aliyekuwa
akiwasafirisha kutoka Ethiopia kwenda Afrika Kusini kwenye eneo la
pembezoni kidogo mwa fukwe ya bahari ya hindi katika kata ya Nianjema.
Kamanda Maro, alisema
matukio ya wahamiaji wanaoingia bila kibali na magendo kupitia Bagamoyo
yamekuwa yakitokea mara kwa mara kutokana na njia za panya hasa bahari
.
Nae mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo, alhaj Majid Mwanga, alisema tatizo la kuingia kwa wahamiaji
haramu katika mwambao wa bahari ya Hindi na kupitia bandari bubu zilizo
wilaya hiyo.
Akizungumza baada ya
kupatiwa taarifa hiyo, mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Ndikilo, alitoa
onyo kwa watu wanaofanya biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu .
Mhandisi Ndikilo, alibainisha wasafirishaji hao waache tabia hiyo mara moja kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment