Mahabusu
wanaotuhumiwa na ugaidi jijini Arusha leo baadhi yao wamegomea kushuka katika
gari la magereza
kwa madai
kuwa hawatendewi haki kwa kesi zao kutosikilizwa hali inayowalazimu kukaa
mahabusu kwa muda mrefu bila kujua hatima yao
Watuhumiwa wa ugaidi baadhi yao wakiingia katika gari la magereza baada ya 32 kutii amri ya mahakama
Watuhumiwa wa ugaidi wakiwa katika viwanja vya mahakama leo jijini Arusha
Na Pamela Mollel,Arusha
Katika hali
isiyokuwa ya kawaida Mahabusu
wanaotuhumiwa na ugaidi jijini Arusha baadhi yao leo wamegomea kushuka katika
gari la magereza kwa madai kuwa hawatendewi haki kwa kesi zao kutosikilizwa hali
inayowalazimu kukaa mahabusu kwa muda mrefu bila kujua hatima yao
Tukio hilo
lilitokea katika viwanja vya mahakama
majira ya saa 9:27 asubuhi ambapo tukio hilo lilisimamisha shughuli za mahakama
kwa muda wa zaidi ya masaa mawili huku baadhi ya watuhumiwa wengine wa ugaidi
wakivua nguo zao kushinikiza kesi zao kusomwa
Mahabusu 32
tu ndio waliokubali kushuka katika gari hilo na kuingia mahakamani huku 29
wakigomea kushuka na kubakia ndani ya gari hali iliyozua taharuki kwa baadhi wa
watu walikuja kufatilia kesi hiyo
Hakimu mkazi
wa mahakama hiyo Nestory Baro aliwataka watuhumiwa hao kuwa wavumilivu, kwa
kuwa kesi yao ipo katika hatua za mwisho huku akiwasii kutogomea kuja mahakamini
kwa kufanya hivyo wanajinyima haki yao ya kisheria
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti mahakamani hapo watuhumiwa hao Shabani Idi na Yusuph Alli
waliiomba mahakama kuharakisha kesi hiyo kwa kuwa familia zao zinaishi katika
wakati mgumu
“Mtoto wangu
wa darasa la nne amekatisha masomo anaokota makopo kwaajili ya kuuza ili
familia wapate chakula pamoja na wadogo zake kupata nauli ya shule”alisema
Shabani
Aidha
waliongeza kuwa familia zao sasa zipo hatarini kuingia katika makundi mabaya ya
tabia kutokana na wazazi wao kuwa mbali nao hivyo wao kuendelea kuwepo
magerezani ni changamoto kubwa sana kwa
familia zao
No comments:
Post a Comment