Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford akielezea kwa undani namna shirika hilo litakavyoweza kufanya kazi nchini Tanzania na kuitaja mikakati mitano waliyo iweka kwa ajili ya Shirika hilo.
Mmoja wa Blogger Bw. Bethuel Kinyori ambaye ni Mmiliki wa mtandao wa Dailypulse24.com akiuliza swali wakati wa Mkutano huo ulio fanyika katika Hotel ya New Africa Jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa Habari za Mtandaoni.
Mmoja wa wafanyakazi wa WFP Bw. Masasa Makwasa akielezea namna Programu ya ‘Farm to Market Alliance’ inavyofanya kazi na inavyowasaidia wakulima katika shughuli zao za Kilimo.
Mtaalam wa mambo ya usimamizi wa Fedha ambaye pia ni Blogger Bi. Monica Joseph akiuliza swali linalohusiana na maswala ya fedha hasa kwa wakulima ambao WFP wanaofanyanao kazi.
Bi. Alice Maro kutoka WFP akielezea mambo zaidi kuhusu Shirika hilo
Bw. Krantz Mwantepele ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Koncept na Mmiliki wa mtandao wa Mwanaharakati Mzalendo akiuliza swali wakati wa Mkutano huo.
Baadhi ya Bloggers wakiwa katika mkutano huo
Baadhi ya watumishi wa WFP wakiwa katika Mkutano huo uliowahusisha waandishi wa Habari za Mtandanaoni (Bloggers)
Bw. Masasa Makwasa kutoka WFP akijibu baadhi ya Maswali yaliyoulizwa na Bloggers
Picha ya Pamoja ya watumishi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) pamoja na waandishi wa Habari za Mtandaoni (Bloggers)
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa Tanzania
Habari na Michuzi Media na Mo Blog Shirika la chakula Duniani (WFP) limetambulisha mikakati yake mitano ya
kutokomeza njaa nchini itakayofanyika ndani ya miaka minne kuanzia
mwaka huu hadi 2021.
Akizungumza katika warsha iliyowakutanisha WFP na waandishi wa Habari za mtandaoni, mkurugenzi wa WFP Tanzania,Michael Danford ameitaja mikakati hiyo kuwa, ni kuwasaidia wakimbizi na jamii zao, kutoa msaada wa lishe hasa katika maeneo ya Dodoma na Singida.
Aidha alitaja mikakati mingine kuwa ni, kuimarisha mfumo wa chakula Serikalini na ubunifu wa namna ya kupata chakula cha ziada.
Akifafanua namna ya utekelezaji wa mikakati hiyo, amesema, watatoa
msaada wa fedha kwa wakimbizi wapatao 400,000 kwa ajili ya kuwawezesha kupata mahitaji yao wanayotaka pia kuiongezea serikali kipato.
“Kuna faida zaidi ya kutumia fedha kuliko chakula kwa wakimbizi kwani
kila dola moja iyakayotumika inaweza kuimarisha uchumi wa nchi sababu
fedha zitakazoingia zitakuwa za kigeni”.
Aidha ameongeza, WFP kwa kushirikiana na wadau wengine watatoa elimu kwa wakulima wadogo juu ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuwaunganisha kwenye masoko ya uhakika.
” Tangu Tanzania ipate Uhuru, WFP ndio iliyosaidia wakulima kwa Mara ya
kwanza kupata mikopo kutoka benki, tulikaa na taasisi za fedha
tukawashawishi kuwaamini wakulima na kuanza kuwapa mikopo,” amesema.
No comments:
Post a Comment