Wahitimu
 wa darasa la Saba katika shule ya Msingi Nalopa wakitumbuiza wageni 
mbalimbali wakati wa sherehe ya Mahafali iliyofanyika jana katika 
viwanja vya shule hiyo iliyopo jijini hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa 
Jeshi la Polisi Arusha)
Wazazi
 na Walezi wa wanafunzi wa shule ya Msingi Nalopa wakimsikiliza Kamanda 
wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Mkumbo ambaye alikuwa 
mgeni rasmi kwenye sherehe ya Mahafali ya kuhitimu darasa la Saba (Picha
 na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Mgeni
 rasmi wa sherehe ya Mahafali ya darasa la Saba katika shule ya Msingi 
Nalopa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles 
Mkumbo akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu (Picha na Rashid Nchimbi wa 
Jeshi la Polisi Arusha)
Kamanda
 wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo 
akiwahutubia wageni waalikwa katika sherehe za Mahafali ya wanafunzi wa 
darasa la Saba wa shule ya Msingi Nalopa (Picha na Rashid Nchimbi wa 
Jeshi la Polisi Arusha)
……………………………………………………………..
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Wito umetolewa kwa wazazi, na kuelezwa kwamba mbali na kujitahidi kuwasomesha watoto wao  katika
 shule mbalimbali kwa lengo la kuwapatia elimu bora wametakiwa pia 
kuzingatia kuwapa makuzi mema ili uhalisia wao kimuonekano uendane na 
elimu wanayoipata.
Hayo
 yameelezwa jana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna 
(DCP) Charles Omari Mkumbo wakati wa sherehe ya mahafali ya wahitimu wa 
darasa la saba katika shule ya Msingi Nalopa iliyopo jijini Arusha.
Kamanda
 Mkumbo ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika mahafali hayo alisema kwamba, 
wanafunzi hao kwa sasa wanakwenda katika hatua nyingine ya kimasomo 
lakini pia umri wao unaongezeka na kukumbana na changamoto mbalimbali, 
hivyo wazazi wanatakiwa waendelee kuwakuza kimaadili ili elimu yao iwe 
na manufaa kwao na kwa jamii.
Alisema
 elimu wanayoipata ikiendana na maadili itawasaidia kuepuka kujiingiza 
katika vitendo vya uhalifu kama vile matumizi ya dawa za kulevya na 
uhalifu mwingine wowote na hatimaye kuonekana kuwa wa thamani machoni 
mwa watu.
Kamanda
 Mkumbo aliwataka wanafunzi hao kuongeza bidii katika masomo yao hasa ya
 Sayansi ili idadi ya wataalamu wengi katika kada mbalimbali iongezeke 
hasa katika huu ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia ambao ushindani wa 
soko la ajira umekuwa mkubwa.
Akimkaribisha
 mgeni rasmi kuwatunuku vyetu wahitimu hao ambao walifanya vizuri 
kimasomo, kinidhamu, uongozi, kimichezo na kujituma, Mlezi wa shule hiyo
 Balozi Mstaafu Bw. Daniel Ole Njoolay alitumia nafasi hiyo kumpongeza 
Kamanda huyo  kwa kuzidi kuimarisha hali ya usalama katika mkoa wa Arusha pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo.
Awali
 akizungumza katika Mahafali hayo Meneja wa shule hiyo yenye wanafunzi 
461 Bw. Edward Njoolay alisema kwamba, awali akisoma wasifu wa shule 
hiyo alisema kwamba mwaka 1999 ilikuwa kama “Day Care” lakini ushawishi 
wa wazazi uliwawezesha kufanikiwa kufikia hatua kubwa kimiundo mbinu na 
kitaaluma.
Shule
 hiyo imefanikiwa kutoa wahitimu wa darasa la saba mara nane ukiondoa 
wahitimu wa jana na wote walifanikiwa kufaulu na kuendelea na masomo ya 
Sekondari ambapo mwaka 2016 ilishika nafasi ya saba katika shule bora za
 Halmashauri ya jiji la Arusha zilizofanya mtihani wa darasa la saba.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
.jpeg) 
 
No comments:
Post a Comment