Katibu Tawala Wilaya ya Arusha David Mwakiposa akizungumza leo katika warsha ya siku tatu jijini Arusha iliyowakutanisha watetezi wa
haki za wafugaji nchini , mafunzo hayo yanalengo lakuwajengea uwezo watetezi hao ili waweze kuondoa
migogoro inayojitokeza katika jamii(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)
Mratibu wa mtandao wa watetezi wa
haki za binadamu,THRDC Onesmo Ole Ngurumo alisema kuwa ni vizuri watetezi hao wakajengewa
uwezo katika sera ,sheria na mifumo ya utoaji haki katika taifa hili na nje ya
Nchi ili waweze kutetea vizuri wafugaji
Katibu mkuu
chama cha wafugaji Tanzania Maghembe Makoye alisema kuwa Tanzania inamifugo na
wafugaji wengi hivyo ni muhimu sana sekta hiyo kujengewa uelewa na kujielekeza
kuunda mabaraza ya usuluishi katika ngazi ya vijiji,kata,tarafa hadi wilaya ili
kuhakikisha kundi hilo haligombani
Makamu Mwenyekiti Taifa Esther Laban Alimuomba Rais Magufuli kuangalia namna ya kuwaelimisha zaidi
Na Pamela Mollel,Arusha
Serikali imewaomba
viongozi wa chama cha wafugaji Tanzania pamojana watetezi wahaki za wafugaji
kuhakikisha wanaondoa migogoro ya wafugaji na wakulima ambayo imekuwa
ikijitokeza mara kwa mara Nchini hali ambayo imekuwa ikirUdisha maendeleo nyuma
Akizungumza
jijini hapa katika ufunguzi wa warsha ya siku tatu iliyowakutanisha watetezi wa
haki za wafugaji nchini ,Katibu Tawala Wilaya ya Arusha David Mwakiposa alisema
kuwa lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo hao watetezi ili waweze kuondoa
migogoro inayojitokeza katika jamii
“Serikali
tunaomba sana watetetezi wa haki za wafugaji kuangalia kwa uzito wa kipekee
kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima na wahamasishe uwanzishwaji wa viwanda
vya kuchakata bidhaa za mifugo ili kumuunga mkono Raisi Magufuli katika sera ya
viwanda”Alisema Mwakiposa
Aidha
alisema kuwa sekta ya wafugaji na kilimo inaajiri watanzania walio wengi zaidia
asilimia 70 na ndio sekta pekee ambayo haiitaji elimu kubwa tofauti na ajira za
viwandani na sehemu nyingine hivyo ni muhimu kujengwa uwezo ili kutimiza sera
ya viwanda hapa nchini
Kwa upande wake mratibu wa mtandao wa watetezi wa
haki za binadamu,THRDC Onesmo Ole Ngurumo alisema kuwa ni vizuri wakajengewa
uwezo katika sera ,sheria na mifumo ya utoaji haki katika taifa hili na nje ya
Nchi ili waweze kutetea vizuri wafugaji
“Tunaamini
kuwa watetezi hawa wakifahamu vizu sera na sheria wataweza kuangalia mifumo ya
utoaji haki kama haitendeki kwa wafugaji
wataweza kutumia fursa hiyo kuwatetea vizuri”
Katibu mkuu
chama cha wafugaji Tanzania Maghembe Makoye alisema kuwa Tanzania inamifugo na
wafugaji wengi hivyo ni muhimu sana sekta hiyo kujengewa uelewa na kujielekeza
kuunda mabaraza ya usuluishi katika ngazi ya vijiji,kata,tarafa hadi wilaya ili
kuhakikisha kundi hilo haligombani
“Nivizuri
tukihamasishana kufuga kisasa ili kujiongezea tija katika uzalishaji wa bidhaa
za wafugaji sanjari na kupata masoko ndani na nje ya nchi “
No comments:
Post a Comment