Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na moja ya
wahudumu wa Choo Cha Kituo Cha Mabasi Simi 2000 Mara baada ya ziara ya
kushitukiza kujionea Hali ya ukusanyaji mapato Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua maeneo
mbalimbali ya ukusanyaji Kodi Mara baada ya ziara ya kushitukiza katika
kituo Cha Mabasi Sinza na kujionea Hali ya ukusanyaji mapato Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akimtaza muhudumu wa
kituo Cha Mabasi Sinza Mara baada ya ziara ya kushitukiza katika kituo
Cha Mabasi Sinza na kujionea Hali ya ukusanyaji mapato Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua maeneo
mbalimbali ya ukusanyaji Kodi Mara baada ya ziara ya kushitukiza katika
kituo Cha Mabasi Sinza na kujionea Hali ya ukusanyaji mapato.Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua fedha chakavu
iliyotolewa na mteja Mara baada ya ziara ya kushitukiza katika kituo Cha
Mabasi Sinza na kujionea Hali ya ukusanyaji mapato Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na Watumishi
wa Manispaa ya Ubungo wanaohudu katika kituo Cha Mabasi Sinza na
kujionea Hali ya ukusanyaji mapato.
Na Mwandishi Wetu, Dar as salaam
Afisa Mapato wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg Fulgence Rweyagaza ametakiwa
kujitathmini Kama anafaa kuendelea na majukumu yake ama vinginevyo
kutokana na kushindwa kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato ya Manispaa
katika Kituo Cha Mabasi Simu 2000 kilichopo Kata ya Sinza.
Agizo Hilo limetolewa
Jana June 23, 2017 na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi
Kayombo Mara baada ya ziara ya kushitukiza katika kituo Cha Mabasi Sinza
na kujionea Hali ya ukusanyaji mapato isivyo na weledi.
MD Kayombo amebaini
kutotolewa risiti ipasavyo ambapo Jambo Hilo limetajwa kuwa ni moja ya
sababu ya kupatikana mapato kiduchu ukilinganisha na huduma zinazotolewa
Kwa wananchi.
Akiwa kituoni hapo MD
Kayombo aliamua kutumia zaidi ya masaa matano kusimama mwenyewe
dirishani kukusanya fedha za watu waliokuwa wanapatiwa huduma ya Choo
ambapo kwa muda wote huo amebaini uwepo wa fedha nyingi ambazo zilikuwa
zinapotea.
Kituo Cha mabasi cha Simu 2000 kina maeneo matatu ya ukusanyaji mapato ambapo ni Choo, Soko pamoja na Daladala.
Katika hatua nyingine MD
Kayombo amewafuta kazi watumishi wawili wa kujitolea ambao wamekosa sifa
ya kuendelea kuwa wasaidizi katika kazi za Kituo hicho.
No comments:
Post a Comment