Mch.Dr.Jerry Williamson
kutoka nchi Marekani akiomba katika ibada ya katika kongamano kanisa la
Zion lililopo njiro jijini Arusha ambapo kanisa hilo limeendaa semina na
kongamano kwa wachungaji pamoja na washirika wengine,kulia kwake ni
Ben Mangeni ambaye ni mkalimani wake
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo
Mch.George Mngodo akiongea na waandishi wa habari , alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki kongamano hilo wataweza kujifunza
mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine
Mmoja wa wachungaji wa
kanisa hilo Paul Sulley akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi
anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa bidii.
kushoto ni Mtume trice Shumbusho akiwa na mkalimani wake akihubiri katika kongamano hilo
Waumini wakiwa katika maombi
Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwaajili ya kongamano
Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwaajili ya kongamano
Picha ikionyesha madhabahuni
Picha ikionyesha jengo la kanisa
Picha ikionyesha jengo la kanisa
Na Pamela Mollel,Arusha
Wachungaji zaidi ya 300
kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini bila kujali madhehebu yao wako katika semina maalumu ya neno la Mungu yenye
lengo la kusaidia kupeleka ujumbe wa madhihilisho ya nguvu ya kristo katika maeneo
mbalimbali ya nchi ili watu waweze kubadilika na kumjua Mungu
Semina hiyo ya siku
nane iliyoandaliwa na kanisa la Zion City Church Arusha litafanyika
kanisani hapo ikiambatana na Kongamano ambalo limeandaliwa kwa ajili ya wachungaji na
watu mbalimbali likiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kupeleka injili kwa watu
wa mataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya kongamano hilo Mch.George Mngodo alisema kuwa watu ambao wataweza
kushiriki wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo
yatawawezesha kuvuka kutoka hatua moja
kwenda nyingine.
Mngodo aliongeza kuwa huduma zitakazo tolewa katika katika
kongamano hilo hazitawakugusa kiroho tu bali hata kwenye maisha yao ya kawaida
wataweza kubadilika
“Tunaamini kongamnao
hili litagusa wachungaji hawa na jamii wanayoihudumia kimwili na kiroho”alisema
Mngodo
Kwa upande wake mmoja
wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley alisema kuwa matarajio yao ni kuona
kila mtumishi anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa bidii.
Mch.Sule alisema kuwa ulimwengu
wa sasa umeharibika hivyo unahitaji watumishi waliokutana na Mungu na si
wanaomjua Mungu pekee ili waweze kuwatumikia watu.
Miongoni mwa watumishi
wa Mungu wa kimataifa watakao kuwa wasemaji wakuu katika kongamano hilo ni Askofu
mkuu wa kanisa la Zion City Church Arusha John
Shumbusho pamoja na mkewe Trice Shumbusho
Wachungaji
wengine ni kutoka nje ya nchi Mch.Dr.Jerry
Williamson, Mch.Dr Jim Oxendine kutoka Marekani,Mch.Yoshua Masasu kutoka
Rwanda,Mch.Aloysius Kiiza kutoka Uganda,Pamoja na Mch.George Mkandawire kutoka Afrika
Kusini .
No comments:
Post a Comment