Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb)amabye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika uzinduzi wa baraza la pili la Wafanyakazi wa chuo cha Uhasibu Arusha,alisema madhumuni ya baraza hilo ni kuwapa fursa watumishi kupitia wawakilishi wao pamoja na kujadiliana juu ya masuala mbalimbali.(Habari Picha na Pamela Mollel)
Makamu Mweneyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha
Bw.Juma Kaniki akisoma risala katika uzinduzi huo
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi akiteta
jambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro katika uzinduzi wa
baraza la pili la wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha
Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb)katikati akinyoosha juu mkataba wa kuunda baraza ambao umehakikiwa na kusainiwa na Kamishna wa kazi,wa pili kulia niKaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi,na wakwanza kushoto ni Didas Malekia Mwenyekiti wa tawi la IAA chama kilichounda baraza la wafanyakazi(THTU)
Baadhi ya wanafunzi chuo cha Uhsibu Arusha wakifatilia hotuba ya mgeni
rasmi kwa umakini ambapo pamoja na mambo mengi Naibu Waziri wa fedha na Mipango
Dkt.Ashatu Kijaji aliwasisitiza umuhimu wa kila mmoja kuwa mshiriki mkubwa wa
kupambana na rushwa ambayo inajikita katika kupotosha na kumomonyoa maadili.
Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb)
akiwa katika picha ya pamoja na baraza la wafanyakazi wa chuo cha Uhasibu
Arusha Tarehe 10 Januari 2018
No comments:
Post a Comment