Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akinunua
moja ya mkoba uliotengenezwa na kikundi cha Jauki kwenye banda la Halmashauri
ya Wilaya ya Kilwa mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya 24
ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya
Manispaa ya Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akimtazama
mnyama aina ya kakakuona wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane
katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akitembelea
mabanda mbalimbali ya wajasiriamali wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane
katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi
Baadhi ya Wajasiliamali wakimsubiri Mkuu wa Mkoa wa
Lindi Mhe Godfrey Zambi kutembelea katika banda lao wakati wa Maonesho ya 24
ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya
Manispaa ya Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akionyesha
Dawa aina ya Mlonge inayotibu magonjwa mbalimbali wakati wa Maonesho ya 24
ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya
Manispaa ya Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akikagua
baadhi ya viatu vilivyotengenezwa na wajasiriamali wakati wa Maonesho ya 24
ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya
Manispaa ya Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akikagua
banda la Wakala wa vipimo wakati wa Maonesho ya 24
ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya
Manispaa ya Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akisaini
kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Viwanda, Biashara na
Uwekezaji wakati wa Maonesho ya 24
ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya
Manispaa ya Lindi
Na
Mathias Canal, Lindi
Taasisi mbalimbali za fedha nchini zimeshauriwa kuwa
na masharti nafuu ya utoaji mikopo ili kuwarahisishia wajasiriamali kuwa na
fursa rahisi ya kupata mitaji kwa minajili ya kuendeleza biashara zao.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi amesema hayo
wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda
mbalimbali ya Maonesho ya 24
ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya
Manispaa ya Lindi.
Katika
Maonesho hayo yenye kauli mbiu ya “Zalisha
kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati”
wananchi watapata fursa yatawasaidia wananchi kupata wananchi watapata elimu
ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa muda mfupi lakini pia wadau kujionea
na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, mashirika ya umma na binafsi
Mhe Zambi alisema kuwa miongoni mwa changamoto
ambazo zimekuwa mwiba mcvhungu kwa wajasiriamali ni pamoja na namna ya kupata
mitaji kutoka katika taasisi mbalimbali za fedha jambo ambalo linarudisha nyuma
maendeleo ya biashara.
Alisema mikopo kutoka benki inatolewa kwa masharti
makubwa na riba kubwa jambo ambalo ni kikwazo kwa wajasiriamali ambao wana
mitaji midogo lakini inarudisha nyuma ufanisi wa wao na taifa kwa ujumla wake.
Alisema kuwa Sera ya nchi inaruhusu sekta binafsi
kuendesha uchumi kupitia kampuni ndogo, za kati, na wajasilimali, hivyo mitaji
kwa wajasiriamali ni jambo ambalo haliepukiki.
Zambi alisema kuwa wajasiriamali wakipatiwa huduma
za fedha na kukuza mitaji yao, wana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo ya mtu
mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Zambi amesifu maandalizi mzuri ya Sherehe hiyo
inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kuhusisha
Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja kwa wote wanaoshughulika na kilimo.
Maonesho
ya sikukuu ya wakulima Nanenane yanahusisha shughuli za wakulima, wafugaji wa
mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za
mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi,
mabenki, Taasisi za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa
mayai, Kuongeza thamani ya mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, ambapo
Taasisi za elimu zitaonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili,
Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta.
No comments:
Post a Comment