Wasichana
8,000 waliopo shuleni na 600 ambao hawako shuleni watanufaika na mradi
mkubwa wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupata elimu. Mradi
huo wa miaka minne wenye gharama ya dola za Marekani milioni 5
utafanyika katika wilaya tano nchini. Wilaya hizo ni Ngorongoro, Kasulu,
Sengerema, Micheweni na Mkoani. Mradi huo ambao upo hatua ya pili
umeanza kwa kongamano lililofunguliwa jana na Katibu Mkuu wizara ya
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Leonard Akwilapo. Mgeni
rasmi kwenye kongamano hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo akifungua rasmi kongamano la viongozi
mbalimbali wa wizara na wilaya tano nchini kujadili na kupanga mikakati
ya namna bora ya kuwawezesha wasichana na wanawake vijana katika wilaya
husika kupata elimu katika kipindi cha miaka minne ijayo.
Mradi
huo mkubwa kwa mujibu wa Katibu mkuu huyo umelenga kuwaokoa wanafunzi
kabla hawajakumbwa na matatizo yanayokatisha masomo yao. Aidha utawapa
fursa za kuboresha zaidi mafunzo mbalimbali waliyonayo ambao utawafanya
kuwa watu wazuri zaidi katika jamii na hivyo kuchangia maendeleo ya
taifa na jamii walizopo.
Katibu
mkuu huyo ambaye alifungua kongamano na kuzindua mradi huoi awamu ya
pili alisema kwamba ni matumaini yake kwamba jamii itaukumbatia mradi
huo ili kuwa na taifa lenye mafanikio makubwa katika malengo ya
maendeleo endelevu ya dunia kwa kuzingatia lengo namba tano. Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akitoa
neno la ufunguzi katika kongamano la viongozi mbalimbali wa wizara na
wilaya tano nchini kujadili na kupanga mikakati ya namna bora ya
kuwawezesha wasichana na wanawake vijana katika wilaya husika kupata
elimu katika kipindi cha miaka minne ijayo.
Amewataka
wazazi na vijana kutimiza wajibu wao kwa kubadilika kitabia na kutambua
umuhimu wa elimu katika kufanikisha wanachotaka ambacho ni maendeleo
binafsi , familia na taifa kwa ujumla. Katika hotuba yake alisema ni
matumaini kwamba wadau katika mradi huo watafaikisha katika kipindi cha
miaka minne mipango yote iliyolenga kuboresha huduma kwa wasichana na
wanawake vijana, kushawishi jamii kubadilika na kuachana na tamaduni
mbaya kama ndoa za utotoni na ukeketaji.
Naye
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni
UNESCO, Zulmira Rodrigues alisema mradi huo ulioanza mwaka jana na
kufanyiwa tathmini umeonesha changamoto kubwa ya watoto wa kike ikiwamo
mimba za utotoni,ukeketaji na kushindwa masomo. Mkurugenzi
wa Shirika la Kimataifa la misaada Korea International Cooperation
Agency (KOICA) nchini, Joonsung Park akitoa neon kuhusu ufadhili wa
KOICA ambao imeutoa katika mradi huo na mipango yao ya kusaidia
Tanzania.
Alisema
lengo la mradi ni kuhakikisha kwamba mwanamke anapata fursa za
kupambana katika mazingira yake kama anavyofanya mwanaume kwa kuwezeshwa
na kuzuia mila, tabia na tamaduniu mbaya ambazo zinakwamisha uwezo wake
wa kuhudhuria masomo.
Aidha
alisema mradi huo utatoa nafasi kwa wanawake vijana ambao wamekosa
masomo au wameacha masomo au hawakwenda shule kabisa kupata nafasi ya
kusoma. Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la kimataifa la misaada la
Korea (KOICA) kupitia UNESCO na kufanyiwa kazi pia na mashirika ya UN
Women na UNFPA unaangalia namna bora ya kukabiliana na changamoto za
mabinti wanaokwenda shule katika wilaya hizo ili kuwawezesha kuwa watu
bora katika jamii siku za usoni. Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA)
nchini, Dk. Hashina Begum akitoa neno kwa niaba ya UNFPA.
Mradi
huo ni sehemu ya mradi wa Global Initiative unaoendeshwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, sayansi na Utamaduni (UNESCO), Shirika la
Mpango wa watu (UNFPA) na Shirika la Umoja wa mataifa la wanawake(UN
Women) wa kuwawezesha wanawake kupitia elimu uliozinduliwa katika nchi
sita duniani. Awamu ya kwanza ya mradi huo umelenga kufanywa katika nchi
tatu za Mali, Nepal na Tanzania na ulitiwa saini mwaka jana, 2016.
Katika mradi huo serikali ya Tanzania inawakilishwa na Wizara ya Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi; Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Katiba na Sheria ambayo
ikiratibu mradi kwa niaba ya serikali ya Tanzania. Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Tanzania, Bi. Hodan Addou akitoa neno kwa niaba ya UN Women.
Aidha
UNESCO inatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na UNFPA na UN Women.
Katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa KOICA Tanzania, Joosung Park pia
alizungumza umuhimu wa kufundisha watoto wa kike na kuwapa fursa na
kusema kwamba unapofunza wanawake unafunza taifa huku akisema kwamba
wazazi wanahusika sana katika hilo akitolea mfano waziri wa mambo ya nje
wa Korea wa sasa ambaye ni mwanamke kwa mara ya kwanza katika miaka
mingi ya historia ya nchi hiyo.
Mzungumzaji
mwingine ni ambaye alikuwa Mwakilishi wa UNFPA Tanzania, Dk Hashina
Begum alitaka jamii kuhakikisha kwamba inatoa elimu ya afya ya uzazi kwa
vijana ili kuzuia uzazi usiokuwa na mpango ambao unakwamisha maendeleo. Anna
Holmström kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) akitoa maelezo kuhusu mradi huo kwa
washiriki waliohudhuria kongamano hilo.Picha juu na chini ni Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo. [Washiriki
wa kongamano la viongozi mbalimbali wa wizara na wilaya tano nchini
kujadili na kupanga mikakati ya namna bora ya kuwawezesha wasichana na
wanawake vijana katika wilaya husika kupata elimu katika kipindi cha
miaka minne ijayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment