Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki
Ulisubisya akizungumzxa na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa nne wa`masuala ya Ganzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Waandi wa habari
wakimsikiluliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya
leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
*****************
SERIKALI yaja
na mpango mkakati wa kudumisha matibabu ya uzazi pingamizi ili kupunguza vifo
vya wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchini Tanzania.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati waa ufunguzi wa
mkutano wa nne wa`masuala ya Ganzi uliofanyika jijini Dar es salaam.
“Huwezi kutoa huduma bora na salama ya uzazi pingamizi bila kuwa na wataalamu wa
ganzi ili kufanywa upasuaji usio na maumivu hivyo katika mkutano huu tunapanga
kuwa na wataalamu wengi wa huduma hiyo ili kutoa huduma bora nchini.
Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa licha ya
kudumisha matbabu ya uzazi pingamizi pia Serikali imejidhatiti kujenga vituo
vya afya vinavyotoa huduma hiyo kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa
ujumla.
Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mkutano
huo unalenga kutoka na malengo ya kutoa huduma bora kwa wagonjwa mahututi
pamoja na kutoa huduma ya ganzi kwa wanaohitaji kupasuliwa.
Mkutano huo ulioandaliwa na Chama cha Wataalam Wa
Ganzi nchini (SATA) umeudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Sweden,Cameroon,
Marekani , Tanzania ili kuweza kujua
mchango wa kupunguza vifo vya wajawazito kutokana na huduma ya ganzi.
No comments:
Post a Comment